Wakili wa Jamhuri, Joseph Pande alisimama na kupinga kwa shahidi huyo kuwa wa kwanza huku akisisitiza kwamba katika utetezi huo, watuhumiwa ndiyo wanaopaswa kuanza.
Kimsingi anayetakiwa kuanza ni mtuhumiwa kujitetea na kama atakuwa na mashahidi ndipo wataitwa hao mashahidi wake. Sasa hii itakuwa ni jambo la ajabu kutokea kama ataanza shahidi tofauti na mhusika mkuu (mshtakiwa),” amesema Pande.
Msanii Diamond Platnumz leo Februari 8, 2018 amekumbana na maswahibu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu alikokwenda kusikiliza kesi inayomkabili ya matunzo ya mtoto Prince Abdul, baada ya moja ya kiatu chake cha wazi kukatika.
Baada ya tukio hilo, msanii huyo amelazimika kukaa katika moja ya mabenchi yalipo katika mahakama hiyo, kusaidiwa na mmoja wa watu alioongozana nao kukiweka sawa kiatu hicho.
Ufundi huo wa aina aina uliofanywa na msaidizi huyo wa Diamond, ulichukua takriban dakika tano kisha kumkabidhi msanii huyo kiatu hicho ambacho alikivaa na kuingia ndani ya chumba cha mahakama.
Diamond, yupo mahakamani hapo upande wa watoto kusikiliza kesi inayomkabili ya matunzo ya mtoto Prnce Abdul iliyofungulizwa na mwanamitindo Hamisa Mobeto.
Wizara ya Mambo ya ndani ya Nchi imesema sheria haijaweka masharti ya askari wa jinsia gani anatakiwa kufanya upekuzi wa makazi ya nyumba yenye mke na mume.
Kauli hiyo imetolewa leo Februari 8, 2018 bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri wa wizara hiyo, Hamad Masauni wakati akijibu swali la mbunge wa Kojani Hamadi (CUF), Salim Maalim.
Masauni amesema licha ya kuwa sheria haipo, polisi kwa kutumia kanuni za kudumu za Jeshi la Polisi (PGO) pia kwa kuzingatia busara na utu wa mwanadamu, huwa inazingatia busara na utu wa mwanadamu.
Kuhusu upekuzi amesema kifungu cha 38 cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai sura 20 inatoa masharti ya utaratibu wa upekuzi kwenye maeneo mbalimbali ikiwamo nyumba, majengo na vyombo vya usafiri kama magari na boti.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.