Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

ba646be980f9243aa772b9cbb591b59d.jpg
 
Klabu ya Barcelona Jana usiku imefanikiwa kutinga fainali ya Kombe la Mfalme nchini Hispania (Copa del Rey) kwa kuicharaza klabu ya Valencia goli 2-0.
 
Magoli ya Barcelona yamefungwa na Ivan Rakitic na mshambuliaji mpya wa Barcelona Philippe Coutinho ikiwa ni goli lake la kwanza tangu ajiunge klabuni hapo akitokea Liverpool.

Barcelona wamefanikiwa kufuzu kwa aggregate ya magoli 3-0 baada ya mchezo wa kwanza Barca kushinda goli 1-0.

Barcelona itakutana na Sevilla kwenye mchezo wa fainali ya Kombe la Mfalme itakayochezwa Aprili 21, 2018.
 
Hii inakuwa fainali ya 5 mfululizo kwa Barcelona ambapo imeweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza Hispania kucheza fainali nyingi mfululizo na wamefanikiwa kuchukua kombe hilo mara nne.
 
Hii inakuwa fainali ya 5 mfululizo kwa Barcelona ambapo imeweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza Hispania kucheza fainali nyingi mfululizo na wamefanikiwa kuchukua kombe hilo mara nne.
 
Mchezaji mpya wa klabu ya Manchester United Alexis Sanchez amehukumiwa jela miezi 16 kutokana na kosa la kukwepa kulipa kodi.
Hukumu hiyo imetolewa jana ,Sanchez anadaiwa kukwepa kulipa kodi wakati alipokuwa nchini Uhispania ambapo mamlaka nchini humo zinasema anadaiwa kiasi cha pauni laki tisa.
Kwa mujibu wa sheria za Hispania, hukumu ya kosa hilo haizidi miaka miwili jela, lakini badala yake kulipa pauni 525,000 kutokana na kosa ambalo alilifanya miaka mitatu alipokuwa akichezea klabu ya Barcelona.
 
Hukumu ya Sanchez imekuja katika kipindi ambacho bado mamlaka za mapato nchini Hispania zinafanya uchunguzi kuhusu kocha Jose Mourinho anaye tajwa kufanya kosa kama hilo.
 
Kocha wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amelalamika kwamba wachezaji wa Uingereza wamekuwa na tabia ya kujirusha na kutengeneza adhabu. Amesema mchezaji wa Tottenham Dele Alli alifanya kitendo hicho kwenye mchezo wa jumapili huko Liverpool na kusababisha mwamuzi kutoa adhabu ya penalti.
Mchezaji mwingine ambaye anatuhumiwa kufanya kitendo hicho ni Harry Kane, alifanya hivyo kwa mchezaji Virgil van Dijk wa Liverpool na kusababisha mpira wa adhabu
 
Wenger amesisitiza kwamba anakumbuka kumekuwa na kesi za wachezaji kutoka nje ya Uingereza, lakini wachezaji wa Uingereza sasa wameiga tabia hiyo na wamekuwa vinara wa matukio hayo kuliko wachezaji wengine.
 
Siku 10 baada ya Rais John Magufuli kuzindua hati ya kielektroniki ya kusafiria, Idara ya Uhamiaji imetoa maelekezo ya kujaza fomu za maombi kwa njia ya mtandao.
 
Msemaji wa Uhamiaji, Ally Mtanda amesema leo Februari 9, 2018 kuwa fomu hizo zipo kwa Kiswahili na kusisitiza kuwa mwombaji anapaswa kuwa na kitambulisho cha Taifa ili kukidhi moja ya sharti muhimu.
 
Maombi kwa sasa ni mengi, changamoto ni baadhi ya waombaji kutokuwa na vitambulisho vya Taifa ambavyo sasa wanaona umuhimu wake na kulazimika kuvifuata Nida (Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa),” amesema Mtanda.
 
Pia, amesema muda ambao utatumika hadi mwombaji kupata hati yake ya kusafiria ni chini ya siku 14 za kazi ingawa hakubainisha ni siku ngapi.
 
Pili, mwombaji atapaswa kuchagua fomu ya maombi ya hati. Tatu, kuchagua ombi jipya, nne, atatakiwa kutiki kiboksi kukubaliana na maelekezo na tano anaanza kujaza taarifa zake kwa ukamilifu ukifuata maelekezo na mpangilio katika kila kipengele.
 
Back
Top Bottom