Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

HABARI moto moto kwa mashabiki wa soko la burudani ni kwamba, kuna hali ya kutokuelewana kati ya Kanye West na mkewe, Kim Kardashian.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari, ukiwamo mtandao maarufu wa TMZ ni kwamba, mtoto wao mpya aliyezaliwa na mwanamke mmoja aliyepandikiziwa mbegu ndiye chanzo cha varangati hilo.

Iko hivi, kuna mtu amewashauri wanandoa hao kuzitumia picha za ‘kichanga’ hicho katika dili za matangazo, jambo ambalo Kim amekubaliana nalo kwa asilimia 100.

Lakini sasa, wakati Kim akifikiria dili hilo litawaingizia mpunga mrefu, mumewe Kanye amegoma, akisema hataki mtoto wake huyo atumike katika biashara hiyo.
 
Lakini unaweza kujiuliza kwa nini maji ya madafu yanapendwa sana na baadhi ya watu. Jibu ni moja tu, licha ya kinywaji hicho kuburudisha na kupunguza hali ya uchovu wa mwili lakini pia kwa wale wenye mning’inio wa pombe (hangover) huwasaidia kuondosha hali hiyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…