Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Sehemu za Antaktiki
Safu ya Milima ya kuvukia Antaktiki (kwa Kiingereza Transantarctic Mountains) inagawa bara katika sehemu mbili za Antaktiki Magharibi na Antaktiki Mashariki. Mpaka huu unalingana takriban na longitudo ya 180.
 
Antaktiki Magharibi ni upande mdogo zaidi. Ndani yake inagawiwa kwa rasi kadhaa kwa hiyo ina athira ya tabianchi kutoka bahari. Hata kama sehemu kubwa inafunikwa na barafu halijoto haishuki chini mno jinsi ilivyo upande wa mashariki. Rasi kubwa ni Rasi ya Antaktiki (ing. Antarctic Peninsula)
 
Antaktiki Mashariki inafanana zaidi na nusutufe, hakuna rasi au hori kubwa. Kwa hiyo tabianchi ni zaidi ya kibara. Uso unafunikwa na ganda la barafu lenye unene wa kilomita 1.6 au zaidi. Halijoto ya duni inayojulikana ilipimika mwaka 1983 kuwa sentigredi 89,4 chini ya sifuri.
 
Visiwa kadhaa vinahesabiwa kuwa sehemu za Antaktiki. Baadhi ya visiwa hivyo viko ndani ya maji ya bahari. Vingine vinafunikwa na barafu ya kudumu na hivyo haionekani mara moja ya kwamba kuna kisiwa, maana sehemu nyingi ngao nene ya barafu ya kudumu inaingia baharini nje ya pwani.
 
Visiwa hivi ni pamoja na

Kisiwa cha Alexander ambacho ni kisiwa kikubwa cha Antaktiki; kina upana wa kilomita 200, urefu wa kilomita 378 na eneo la km² 49,070. Kinatengwa na bara kwa mfereji wa bahari mwenye upana wa kilomita 24-60, lakini yote inafunikwa kwa barafu ya kudumu ila tu sehemu ya pwani inaiongia katika maji ya bahari.
 
Kisiwa cha Berkner ambacho ni kisiwa kikubwa cha pili chenye urefu wa 320 km, upana wa 135 km na eneo la km² 43,873. Kinafunikwa kabisa na ngao ya barafu, hakionekani hata kutoka baharini.
Visiwa vya Joinville, Roosevelt, Ross na kadhalika.
 
Milima mingi ni sehemu ya Safu ya Milima ya kuvukia Antaktiki (au: milima transaktiki) ambayo ni safu ndefu yenye urefu wa kilomita 3,500 na kufikia kimo cha mita 4500 na zaidi. Ncha za milima yake mirefu zinaonekana juu ya uso wa ngao ya barafu inayofunika bara lote. Mlima mrefu katika safu hii ni Mlima Kirkpatrick wenye urefu wa mita 4528 juu ya UB.
 
Kuna pia volkeno kadhaa, nyingine zimelala, nyingine ziko hai. Volkeno hai ndefu inayotema moto barani ni Mlima Erebus wenye kimo cha mita 3,794: iko kwenye kisiwa cha Ross.
 
Tabia ya pekee ya Antaktiki ni ngao ya barafu inayofunika karibu uso wote wa nchi yake pamoja na sehemu za bahari ya karibu. Ngao ya barafu hii ni mkusanyiko mkubwa wa barafu duniani. Unene wake (yaani kimo juu ya ardhi) unafikia hadi mita 4,500.
 
Ngao ya barafu inajumlisha

asilimia 90 ya barafu yote duniani
asilimia 70 ya maji matamu yote duniani
Ni asilimia 2-3 za eneo lote la bara zisizofunikwa na barafu, yaani km² 280,000 tu.
 
Ngao hiyo ilianza kutokea miaka milioni kadhaa iliyopita. Uzito wake ni mkubwa na inaaminiwa ya kwamba bara lote lilishuka chini kiasi na kama siku moja ngao ya barafu itapotea litapanda tena juu mita kadhaa.
 
Tabia ya pekee ya Antaktiki ni pia uhaba wa mito. Mito yote inayotokea ni ya maji ya barafu ya kuyeyuka wakati wa "majira ya joto" katika miezi ya Februari na Machi. Katika sehemu nyingine ya mwaka mito yote inaonekana kama kanda la barafu. Mto mkubwa ni Onyx unaofikia urefu wa kilomita 30 ukiishia katika Ziwa Vanda.

Mito haina samaki, lakini katika ile mikubwa zaidi kuna mikrobi na algae.
 
Back
Top Bottom