Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kuna maziwa kadhaa chini ya ngao ya barafu. Hata kama jotoridi yake ni chini ya sentigredi 0 baadhi yanaweza kuwa na maji ya kiowevu kwa sababu shinikizo kubwa ya ngao ya barafu linashusha halijoto ya kugandisha maji, hasa kama maji ni ya chumvi.
 
Barafu ya ngao haikai kimyakimya lakini yote ina mwendo ikifuata mtelemko wa uso wa nchi. Katika sehemu kadhaa barafu ina mwendo wa haraka zaidi na sehemu hizi zinaitwa "mito ya barafu" na ni aina ya barafuto. Mito ya barafu hii iko yenye urefu hadi kilomita mia kadhaa, upana wa 50 km na unene wa kilomita 2. Mwendo unafikia hadi mita 1.000 kwa mwaka. Pale inafikia kwenye ufuko wa bahari inajenga ulimi wa barafu inayosukumwa katika maji.
 
Antaktiki si nchi wala dola na hakuna wenyeji au wananchi. Lakini madola mbalimbali yalitangaza madai ya kutawala sehemu za eneo lake. Madai haya hayalingani na mara kadhaa kuna mataifa mbalimbali yanayodai sehemu ileile.

Mataifa yanayodai kutawala sehemu za Antaktiki ni pamoja na Argentina, Australia, Chile, Ufaransa, New Zealand, Norwei na Ufalme wa Maungano.
 
Tangu mwaka 1961 kuna Mkataba wa Kimataifa kuhusu Antaktiki unaosimamisha madai yote ya utawala bila kuyafuta. Mataifa yote yana haki ya kuwa na vituo vya kisayansi. Mapatano ya kando yaliweka masharti makali kwa shughuli za kiuchumi na hadi sasa imewezekana kuzuia migodi na uchimbaji wa madini.
 
Bahari Kuu (ing. w😱cean) ni jina linalotumika kutaja jumla ya maeneo makubwa ya maji ya chumvi duniani yanayopakana na kufuatana kama gimba moja. Kwa maana hii bahari kuu inafunika zaidi ya theluthi mbili za uso wa dunia.
 
Eneo hili kubwa huhesabiwa mara nyingi kama bahari kuu tatu yaani:

Bahari Atlantiki kati ya Amerika upande mmoja na Ulaya - Afrika upande mwingine
Bahari Pasifiki kati ya Amerika na Asia
Bahari Hindi kati ya Afrika na Asia.
 
Hizi sehemu tatu hutajwa pia kama "bahari kuu" kwa kuzitofautisha na maeneo madogo zaidi ya maji ya chumvi au sehemu zinazoitwa bahari ya kando. [1]

Wakati mwingine Bahari ya Aktiki na Bahari ya Antaktiki hutajwa kama bahari kuu ("oceans") za pekee.
 
Bahari kuu hushika asilimia 97% ya maji yote duniani. Hadi sasa ni asilimia 5 pekee zilizofanyiwa utafiti kamili. [2] Kiasi cha maji yote kwenye bahari kuu ni takriban kilomita za mjazo bilioni 1.3.
 
Kiasi cha maji baharini kinajulikana kuwa kilicheza na kubadilika katika historia ya dunia. Wakati wa vipindi vya baridi duniani, kama vile enzi ya barafu, sehemu kubwa ya maji yalipatikana kwa umbo la barafu na maji kiowevu yalikuwa kidogo. [3]. Kuongezeka kwa halijoto duniani kunasababisha kupanda kwa uwiano wa bahari kote duniani. Nchi mbalimbali hasa kwenye pwani au nchi za visiwa zitapungua kieneo.
 
Maji ya chumvi ni maji yenye kiasi cha myeyusho wa chumvi ndani yake. Kwa kawaida kila aina ya maji huwa na kiwango cha chumvi iliyoyeyushwa. Mwili wa binadamu huwa na kiasi cha chumvi ndani yake kwa hiyo hatusikii chumvi kidogo katika maji au chakula.
 
Wataalamu mara nyingi hutaja kiwango cha 0.1 % kuwa maji matamu, kiwango juu ya 1% - 1.5% kuwa maji ya chumvi, na hali ya kati kuwa maji ya chumvi kidogo. Maji ya kunywa yasiwe na zaidi ya 0.1-0.2 gramu chumvi kwa kila lita.
 
Asilimia kubwa cha maji duniani inapatikana kwa umbo la maji ya chumvi kwa sababu bahari kuu ya dunia ina karibu maji yote ya duniani. Maji ya bahari huwa na kiwango cha chumvi cha asilimia 3,5 iliyoyeyushwa ndani yake. Kiwango hiki kinatofautiana kidogo na mazingira. Katika tabianchi ya joto uvukizaji ni kubwa zaidi; maji ya uso wa bahari yanavukiza lakini chumvi inabaki hivyo kiwango cha chumvi ni juu kidogo. Karibu na midomo ya mito maji matamu huchanganywa na maji ya bahari kwa hiyo kiwango cha chumvi inaweza kupungua.
 
Kwa wastani, maji katika bahari ya dunia ina chumvi kwa karibu 3.5% (35 g / L, 599 mM). Hii ina maana kwamba kila kilo (takriban lita moja na kiasi) ya maji ya bahari ina takriban 35 gramu (1.2 oz) ya chumvi zilizoharibiwa (Zaidi ya sodiamu (Na+) Na kloridi (Cl-) Ions). Wastani wa wiani juu ya uso ni 1.025 kg / L. Maji ya bahari ni denser kuliko maji safi na maji safi yana (wiani 1.0 kg / L saa 4 ° C (39 ° F)) kwa sababu chumvi zilizoharibiwa huongeza wingi kwa kiasi kikubwa.
 
Sehemu ya kufungia ya maji ya bahari inapungua kama ongezeko la chumvi linapo ongezeka. Katika salinity ya kawaida, inafungia saa 2 ° C (28 ° F). Maji ya bahari ya baridi (katika hali ya kioevu) ilikuwa mwaka 2010, katika mkondo chini ya glacier ya Antarctic, na kipimo cha -2.6 ° C (27.3 ° F). Maji ya bahari ya pH ni kawaida kwa kiwango cha kati ya 7.5 na 8.4. Hata hivyo, hakuna kiwango cha pH kinachokubaliwa kwa kiwango kikubwa kwa maji ya bahari na tofauti kati ya vipimo kulingana na mizani tofauti ya kumbukumbu inaweza kuwa hadi vipimo 0.14.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…