Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

A) Udongo wa juu: Tabaka ya udongo yenye kiasi kikubwa cha mada ogania ndani yake. Ndani yake kuna minyoo na vijidudu wengi wanaoendelea kula na kubadilisha mabaki ya majani yaliyomo mle kuwa madini au kampaundi ogania sahili zaidi. Kwa kazi yao wanasababisha kuwepo kwa mashimo na nafasi ndogo ndani ya udongo wa juu. Nafasi hizi zinasaidia kuingia na kutoka kwa gesi na kiowevu. Kutokana na uwingi wa viumbehai hivi vidogo udongo wa juu una uwezo wa kutunza maji ya mvua ndani ya nafasi zake. Hii yote ni muhimu kwa kustawi wa mimea inayotandiza hapa mizizi yao.
 
Katika tabaka la udongo wa juu maji ya mvua yanapita haraka zaidi na kwa hiyo madini yeyushi kama chuma, alumini, chumvi mbalimbali na mengine kutegemeana na uwingi wa mvua na hali ya udongo chini yake kiasi cha madini haya yanaweza kuwa haba zaidi.
 
Mmomonyoko (ing. erosion) ni hali ya kuvunjika au kumegekamegeka kwa udongo au mwamba kutokana na athira ya upepo, maji, barafu, joto au mwendo wa ardhi. Kazi za kibinadamu zimekuwa pia sababu muhimu ya mmonyoko.

Katika mazingira yanayokaliwa na binadamu na hasa kwa kilimo mmomonyoko una hatari.
 
Mwendo wa maji ya mito unaweza kuchimba mabonde makubwa. Ukali wake unategemea na kiasi cha maji, kasi yake na aina ya ardhi, kama ina mtelemko mkubwa au kama maji yamepita kwenye ardhi au juu ya miamba. Kama mtelemko ni mkubwa na ardhi ni laini ni rahisi kwa maji kukata bonde ndefu na kubwa.
 
Udongo wote pamoja na mawe madogo unaobebwa na maji hutuamishwa mahali fulani kama mashapo. Kwa njia hiyo maji yanaweza kutenganisha aina mbalimbali za mashapo. Kwa kawaida sehemu nzito hutelemka kwanza na kukaa kama mwendo wa maji unaanza kupungua wakati mto umetoka kwenye mtelemko na kuingia eneo la tambarare. Kwa njia hii aina za mashapo kama vile changarawe, mchanga, matamahuluku na udongo kabisa zinapatikana.
 
Mmomonyoko kwenye mwambao wa bahari au ziwa ni aina ya pekee ya mmomonyoko wa maji. Unatokea hasa kutokana na nguvu ya mawimbi na mikondo. Mikondo ya baharini hubeba muda wote mashapo kwa kuyachukua hapa na kuyatuamisha pale. Kama kiasi kilichochukuliwa kinazidi kiasi kilichotuamishwa mmomonyoko unatokea. Pale panapotuamishwa zaidi kuliko kuchukuliwa fungu linatokea.
 
Barafu ikipatikana kama barafuto (ganda nene la barafu inayoanza kutiririka polepole na kujisukuma mbele)ina uwezo wa kuvunja mawe na miamba mikubwa kabisa na kuzisukuma mbali. Barafuto isipoishia baharini inatoa mito inayoendeleza kazi ya mmomonyoko wa maji.
 
Back
Top Bottom