mambo mrekebisha... samahani mimi ni mdada wa mtoto mmoja, na nina mume pia, Nlikuwa naomba mnishauri kama nipo sawa au sipo sawa, ni hivi mimi ni mtu ambae sipendi mazoea kabisaa, yaani zaidi ntakusalimia tu basi, lakini mazoea ya kukaa vibarazani na majirani ndo siwezagi na nipo hivo tangu mdogo, sipendagi mtu yoyote anizoee sana si unajua mambo ya majirani tena wanavopenda mazoea, kwa hiyo naenda kazini asubuhi na nkirudi najifungia ndani mwenyewe nafanya yangu, wala sitoki.. - - Majirani wengine wanahisi naringa, kumbe ndo nilivyo, sipendagi mazoea ya sanaa,. afu unakuta wana uswahili sana, JAPO NKIPITA NAWASALIMIA VIZURI TU, ILA KUJICHANGANYA NAO KUPIGA STORY NAO VIBARAZANI AU MAJUMBANI KWAO NDO HUWA SIFANYAGI HIVO.... NAOMBA FOLLOWERS WAKO WANISHAURI KAMA NAKOSEA KUWA HIVO AU?