Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mrekebishatabia habari ya shuhuli zako tafathali usinichoke nina tatizo na najihisi nina mkosi nina mwanaume ni rijali ila hawezi kufanya mapenzi na mimi hadi nifosi na ugomvi juu mara nyingi husema kachoka na nikichuna ata mwezi mzima haniombi kabisa mpaka nije nimlazimishe kwa nguvu na nina mfumania sana na wanawake je nina tatizo gani mimi? - - Mwaka wa2 huu na hajawai kunitoa kasoro na anasema ananipenda na nikimfumania anaachana na huyo mwanamke ila lazima awe na mwengine.. Nishaurini
 
Mrekebisha mimi nimeolewa tuna watoto watatu, mume wangu anatoka na msichana wanafanya kazi wote na ofisini kwao wanamjua yeye kuliko mimi. - - Sasa tangu juzi hakurudi nyumbani nikahisi labda issue zake za kikazi maana huwa anapotea hata siku tatu na kwenye simu hapatikani, kumbe alilewa sana na kusababisha ajali akawekwa ndani, leo nimepigiwa simu na shangazi kuambiwa nimeenda kumcheki namkuta yule msichana anayefanya nae kazi ndo anayehangaika kila siku kumletea chakula. Polisi wakaniuliza mimi nani nikasema mkewe wakauliza na huyu ni nani mbona ndo tunajua mkewe? - - Nikashughulika kumtoa ndani Yuko hapa nyumbani kimya haongei nahisi hasira sijui nimfukuze aende kwa yule msichana au niondoke? Na wananangu je? Naombeni ushauri
 
mambo mrekebisha... samahani mimi ni mdada wa mtoto mmoja, na nina mume pia, Nlikuwa naomba mnishauri kama nipo sawa au sipo sawa, ni hivi mimi ni mtu ambae sipendi mazoea kabisaa, yaani zaidi ntakusalimia tu basi, lakini mazoea ya kukaa vibarazani na majirani ndo siwezagi na nipo hivo tangu mdogo, sipendagi mtu yoyote anizoee sana si unajua mambo ya majirani tena wanavopenda mazoea, kwa hiyo naenda kazini asubuhi na nkirudi najifungia ndani mwenyewe nafanya yangu, wala sitoki.. - - Majirani wengine wanahisi naringa, kumbe ndo nilivyo, sipendagi mazoea ya sanaa,. afu unakuta wana uswahili sana, JAPO NKIPITA NAWASALIMIA VIZURI TU, ILA KUJICHANGANYA NAO KUPIGA STORY NAO VIBARAZANI AU MAJUMBANI KWAO NDO HUWA SIFANYAGI HIVO.... NAOMBA FOLLOWERS WAKO WANISHAURI KAMA NAKOSEA KUWA HIVO AU?
 
Wewe ndo wa kuanzisha furaha yako!! Siyo mahusiano yako ndo yakupe furaha, au ndugu zako au marafiki zako... Moyo wako ukiupa furaha.. Kila kitu kitachipuka furaha!! Siku itakuwa na furaha!! Utaambukiza wengine furaha....wewe kwanza, Furaha jipe mwenyewe...
 
NIPO NJIA PANDA... NMECHANGANYIKIWA NAOMBENI USHAURI : . Mimi ni binti nimeolewa kwa miaka mitano sasa, nipo kwenye ndoa na mume wangu na tuna mtoto wa miaka mitatu. Mume wangu ni mtoto wa pekee kwenye familia yao, na kiukweli wako vizuri kipesa, baba yake alishafariki, mwanzo niliona ni kawaida baada ya kuona mama yake ana upendo uliopitiliza kwa mwanae nikiamini kwa kuwa ni mtoto wake wa pekee. Siku nyingine mume wangu akienda kwao anarudi kapendeza kabadili na nguo, ananukia, nikimuandalia chakula hali anasema ameshiba na hata tukilala hanigusi. Nikimlalamikia mama ananiambia kama maisha yamenishinda niondoke kwetu. Juzi nimeshika simu ya mume wangu nilichokiona nilitamani kuzimia, nimekuta meseji akichati na mama yake mzazi akimshukuru kwa mapenzi mazito ambayo hata kwa baba yake alikuwa hayapati. Kiukweli sikuamini kwa sababu ilinifanya nihakikishe namba kama ndio yenyewe kwa kuipiga kwangu na kukuta ya mama mkwe wangu!! Jamani hapa nilipo nipo njia panda, sijui nifanye nini, nikirudi kwetu naona hadi aibu kuelezea kwa familia yangu kwani walimuamini sana. Nifanyeje!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…