Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

b8a9b8e0f1c42458f067fb646699ba6a.jpg
 
Katani ni moja ya mimea ya kale ambayo wanadamu wamekuwa wakiitumia. Katani ilikuwa ndani ya bara la Asia zaidi ya miaka 10,000 iliyopita. Ilikuwa tayari kutumika kufanya nguo, kamba, na aina ya zamani ya karatasi.
 
Katani inafanana na bangi, lakini ina THC kidogo sana, kemikali ambayo huwafanya watu kujisikia vizuri wakati wa kutumia marijuana. Tofauti na marijuana (ambayo sasa inaruhusiwa kisheria huko Colorado), katani inaruhusiwa kisheria nchini Marekani, Ufaransa, Hispania, Indonesia na Uingereza .
 
Mkonge dume ni kiasili mmea wa Meksiko lakini imesambazwa nchi nyingi za kitropiki kutokana na umuhimu wake wa kiuchumi, hasa zao la katani. Kuna mashamba makubwa kwenye kanda la pwani la Afrika ya Mashariki. Kwa miaka mingi Tanzania iliongoza duniani katika zao hilo.
 
Shuke inaanza kama fungu la maua yanayokaa pamoja kwenye sehemu ya shina ya nyasi. Maua haya yanaendelea kuwa matunda yenye mbegu. Mbegu kwa kawaida ni kusudi la kulima mmea na hivyo mashuke ni sehemu za thamani zaidi ya mimea wakati inapovunwa.
 
Njia ya kuvuna ni mara nyingi kukata mashina ya nafaka na kutikisisha au kupiga mashuke hadi mbegu zinaachana na shina na kuzikusanya pekee.

Mashuke hutokea pia kwa manyasi mengine yasiyotumiwa kama nafaka.
 
Maua ni majani ya pekee kwenye sehemu za uzazi wa mimea. Mara nyingi kwa nje huwa na rangi za kuvutia na kwa sababu hii maua yanapendwa pia na wanadamu kama mapambo. Katika lugha ya kila siku neno "ua/maua" linataja pia mmea wote wenye maua.
 
Majani ya nje au petali yanayoonekana vizuri pamoja na rangi yake huitwa petali. Huwa na rangi mbalimbali ili kuvuta wadudu wanaochavusha ua na hivyo kuusaidia mmea kuzaa. Yanaviringisha na kukinga viungo vya uzazi ndani yake.
 
Stameni Edit
Stameni huwa na pande mbili:

Filamenti ni kama shina ya stameni. Juu yake kuna
Chavulio chenye mbelewele ambazo ni seli za kuzaa za kiume.
 
Pistili
Pistili au sehemu ya kike huwa na sehemu tatu:

Stigma ni uso wa kunata juu wa pistili; kazi yake ni kushika mbelewele
Staili inashika stigma na kupitisha mbelewele ndani yake
Ovari ina chembekike ndani yake. Chembekike ni kama yai la mnyama; kikitunganishwa na mbelewele, mbegu unajitokeza.
 
Ovari na mbegu Edit
Baada ya utungishaji ua hukauka na mbegu unakua ndani ya ovari. Kwa mimea kadhaa ovari inaendelea kuwa tunda inayotunza mbegu ndani yake; kusudi la tunda ni kuvuta wanyama wanaokula tunda na kusambaza mbegu kwa njia hii.
 
Mimea mingi huunganisha sehemu za kike na za kiume ndani ya ua moja; mfano ni ua la waridi. Kuna pia mimea yenye maua ambayo ni ama ya kike au ya kiume, kwa mfano maua ya mtango au mboga.
 
Matunda ni sehemu ya mimea kama miti au vichaka vyenye mbegu ndani yake.

Kwa lugha ya biolojia ni ovari ya ua iliyoiva na kuwa na mbegu ndani yake.

Kwa lugha ya kila siku ni zaidi sehemu hiyohiyo kama ina pande zinazoliwa.

Ua la mmea kama imeendelea kukuza mbegu hufunika mbegu mwenyewe kwa ganda la kuukinga. Ganda hili mara nyingi lina sehemu ya nyama ya tunda. Kama sehemu hii ina lishe kwa mwanadamu na ladha ya kupendeza basi ni tunda la kuliwa.
 
Back
Top Bottom