1. Hatari ya kupata magonjwa ya moyo:
Nyama ina kitu kinaitwa lehemu, kitaalamu inajulikana kama cholesterol, hii hukaa kwenye mishipa ya damu ya binadamu na kusababisha damu kushindwa kupita vizuri.
Hii husababisha viuongo muhimu vya mwili kama moyo kukosa damu ya kutosha na kuanza kushindwa kazi. Japokua cholesterol ni muhimu kwenye mwili wa binadamu lakini inayotengenezwa na mwili inatosha hii inayoongezeka kutoka kwenye nyama ni hatari sana.
[nyama nyekundu ina cholestrol nyingi zaidi]

2. Kansa ya utumbo mkubwa:
Nyama nyekundu ikiliwa inakaa masaa ishirini kwenye mfumo wa chakula wa binadamu tofauti na vyakula vingine. Utafiti unaonyesha limbikizo hilo linaambatana sana na hatari ya kupata ugonjwa wa kansa ya utumbo mkubwa. Lakini madhara haya yameonekana kutokuwepo kwa kula nyama nyeupe.
3. Ugonjwa wa kisukari:
Watu wanaokula nyama wameonekana kupata ugonjwa wa kisukari sana kuliko wale wasiokula; na hii ni baada ya kufuatiliwa kwa muda wa miaka kumi mfulululizo [cohort studies]
4. Ugonjwa wa kifafa:
Minyoo inyopatikana kwenye nguruwe kitaalamu kama taenia solium hupanda mpaka kwenye ubongo na kuharibu mishipa ya fahamu ya ubongo hali ambayo husababisha kifafa kwa watu ambao hawakuzaliwa nacho kabisa. Halii hii inaweza kuzuiliwa kwa kupika nyama hiyo kwa muda mrefu sana mpaka iive.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.