Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Miongoni mwa vyakula hivyo ni pamoja na vile vyenye asili ya kijani ambavyo huwa na uwezo mkubwa zaidi katika kuponya magonjwa na kusaidia kujenga mwili na kuimarisha siha.
 
Sehemu kubwa ya miili yetu ni ngozi na ni sehemu muhimu ya mwili ambayo ina jukumu kubwa la kuukinga na kuufunika mwili na viungo mbalimbali, hivyo afya yake pia ni vizuri ikazingatiwa.
 
Vyakula tunavyokula vinaweza kuchangia katika muonekano wa ngozi zetu na kusaidia kupambana na matatizo ya ngozi, ikiwa ni pamoja na kupunguza mikunjano ya uso na suala zima la afya na muonekano wa ngozi.
 
Ni wazi kwamba tuliowengi hupenda kuonekana vizuri, lakini kutokana na kutokuwa na ufahamu sahihi juu ya namna ya kudumisha afya za ngozi zetu kutofahamu njia sahihi za kudumisha afya za ngozi zetu huchangia baadhinyetu kushindwa kufikia lengo na mara nyingine hujikuta tukijisababishia madhara makubwa yasiyotibika hapo baadae.
 
Wataalam wa lishe wanasema kwamba kila tunachokula huwa ni moja ya sehemu ya miili yetu ikiwa ni pamoja na sehemu ya nje, hii inamaana kuwa kila tunavyokula vyakula bora ndivyo ngozi zinavyoonekana vizuri zaidi.
 
Vifuatavyo ni vyakula vinavyoweza kusaidia kuimarisha afya ya ngozi:-

Chakula cha kwanza chenye uwezo wa kuimarisha afya ya ngozi ni asali. Asali ambayo hutengenezwa na nyuki kwa viambato asilia ni chakula muhimu kwa ajili ya kuimarisha afya ya ngozi na pia afya ya binadamu. Hii ni kwa sababu kila kilichokizuri katika afya yako ni kizuri pia kwa ngozi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…