UTANGULIZI
Kabichi ni aina ya mbogamboga ambayo inatunga majani yake kwa kujiviringisha na kutengeneza mduara. Mboga hii inaweza kuliwa bila kupikwa au kuchemshwa kwa kutengeneza kachumbari. Pia inaweza kupikwa pamoja na vyakula kama vile nyama na maharagwe. Kabichi ni chanzo kizuri cha vitamin K, vitamin C na afya kiujumla
ASILI YAKE
Kuna ugumu kuelezea historia ya Kabichi, lakini ni zao ambalo liligundulika na lilikuwa likitumika Ulaya kabla ya miaka 1000 BC. Nchini Tanzania kabichi hustawishwa zaidi katika mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Morogoro, Tanga, Iringa na Mbeya. Kabichi ina madini aina ya chokaa, kambakamba, protini na maji kwa wingi.
HALI YA HEWA
Zao la kabichi hustawi katika mwinuko kati ya mita 1200 hadi 1900 kutoka usawa wa bahari na hali ya ubaridi, pia Udongo ambao ni Tifutifu unaohifadhi unyevu kwa muda mrefu na una Rutuba nyingi na Usiotuamisha maji Usio na chumvichumvi nyingi.Kwa udogo wenye mbolea ya samadi huongeza uzalishaji kwa wingi.
Oxheart
Kabichi zake ni ndogo zilizochongoka mfano wa moyo wa ng’ombe. Zinapendwa sana na walaji kutokana na ladha yake tamu. Hukomaa mapema na hazipasuki.
Oxheart
Kabichi zake ni ndogo zilizochongoka mfano wa moyo wa ng’ombe. Zinapendwa sana na walaji kutokana na ladha yake tamu. Hukomaa mapema na hazipasuki.
Early Jersey Wakefleld
Aina hii inazaa kabichi zenye umbo lililochongoka kidogo (koniko) na zinazofunga vizuri. Kabichi moja inaweza kufikia uzito kati ya kilo 1.5 hadi 2.0. Hukomaa mapema (siku 90 hadi 100) tangu kupandikiza miche.
Prize Drumhead
Vichwa vyake ni vikubwa (Kilo 2.0 mpaka 2.5) na bapa. Huchelewa kukomaa (Siku 110 hadi 120) tangu kupandikiza miche na hupasuka kirahisi. Aina hii huvumilia hali ya jua kali.
Copenhagen Market
Vichwa vya Copenhagen Market ni vya mviringo na hupasuka kirahisi. Aina hii pia hukomaa mapema (siku 90 hadi 100) tangu kupandikiza miche.
Glory of Enkhuizen
Vichwa vyake ni vya mviringo. Aina hii huvumilia hali ya juakali, lakinihuchelewakukomaa (siku 110 hadi 120) tangu kupandikiza miche na haivumilii hali ya kupasuka.
Aina nyingine ni Brunswick na Danish Ball head.
UTAYALISHAJI WA SHAMBA
Unaweza kutumia trecta, jembe la mkono au la ng’ombe kutayarisha shamba, shamba litayarishwe mwezi mmoja kabla ya kupandikiza miche kwa kukatua ardhi hadi kufikia kina cha sentimita 30.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.