UPANDAJI
Upandaji wa Kabichi hufanyika kwa kupandikiza miche ambayo ipo tayari kwa kupandwa shambani, miche huwa tayari kupandwa baada ya wiki 3 – 5 tangu kusia kwa mbegu. Miche huwa na urefu wa sentimita 15 – 20. Ng’oa miche kwa uangalifu na pandikiza kama ilivyokuwa kitaluni na hakikisha mizizi haipindi wakati wa kupandikiza