Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Unawaza Kuacha Ndoto yako au Mpango Wako?

Kuna wakati kila mmoja anafikia hatua ya kutamani kuacha au kukata tamaa katika lengo ulilopanga kulitimiza. Lengo hilo linaweza kuwa na faida kubwa katika maisha yako ya baadae. Lakini kutokana na kuona ugumu wa mpango huo au kukutana na changamoto mbalimbali unaweza kufikia hatua ya kutamani kuacha kuendelea kuamini katika mpango huo. Wengi wanakata tamaa katika hatua hii.
 
Jambo la Muhimu Kutafakari Endapo Ukiwa Unataka Kukata Tamaa

Wakati unapanga malengo yako, ulikuwa na lengo ambalo ulikuwa unaliwaza. Lengo hilo lilikuwa la muhimu sana na ndio sababu ulikubali kupanga jambo lako. Tambua, katika kila mwanadamu aliyefanikiwa kutimiza malengo yake, aliwahi kufikia hatua ya kukata tamaa. Lakini kinachotofautisha wanadamu ambao wametimiza malengo yao na ambao hawajatimiza malengo yao, ni mazoea ya kutokata tamaa.
 
Ukianguka, inuka na endelea na safari!

Safari inaweza kuwa ni ndefu, lakini usikate tamaa. Changamot zipo ili kutufanya wanadamu tuzidi kuwa imara. Mwanadamu anayekuwa na msimamo na malengo yake bila kukata tamaa, ni mwanadamu anayejitambua. Jambo la muhimu ukiwa unataka kukata tamaa jaribu kufanya yafuatayo:
Usifanye maamuzi ya haraka
Tafakari umuhimu wa jambo unalopanga kukata tamaa
Safiri au badilisha mazingira, hii itakusaidia kutuliza akili vyema
 
Kuna Wakati Kukata Tamaa ni Jambo Sahihi

Sio kila jambo linahitaji kushikiliwa sana, ni vyema pia kutambua kuwa kuna wakati ni muhimu kukata tamaa. Hii inatokea pale unapotafakari na kugundua kuwa kuachilia jambo ndio suluhisho. Baada ya kutafakari kwa pande zote mbili, kuangalia faida na hasara za jambo unaweza kugundua kuwa kuna mambo ambayo kuna faida kubwa ukiyakatia tamaa kuliko hasara zake
 
Katika malengo yako, tambua faida za kila jambo na manufaa yake katika maisha yako ya baadae. Kisha weka nia ya kufuata kilicho sahihi katika maisha yako ya baadae. Unapofikia hatua ya kutaka kukata tamaa, chunguza faida na hasara za kukata tamaa. Kisha ukiona njia sahihi au suluhisho sahihi la jambo, lifuate. Tenda kilicho bora katika maisha yako ya baadae.
 
Kumbuka malengo yako kila siku na yape kipaumbele - Paulo Coelho.
Una ndoto na malengo, kila mtu ana malengo na ndoto zake anazofikiria kuzifikia. Kama hauna malengo au mipango utabakiwa kuwa sawa na mtu asiyejua anapaswa kufanya nini.
 
Umeshawahi kujiuliza "Ni kwanini nimezaliwa? Ninapaswa nifanye nini?" Ni dhahiri kuwa haujazaliwa kwa bahati mbaya, umekuja duniani na kupewa akili kwa sababu maalum. Ni vyema kutumia maisha yetu vyema kwa kuchagua malengo sahihi na yanayoendana na sababu na vipaji vyetu katika kuangaza ulimwengu na kuwahamasisha wanadamu wengine kutimiza mwangazao wapo pia.
 
IMANI ZETU HUUMBA UHALISIA WETU.
Mawazo yetu, fikra zetu, misimamo yetu, ufahamu na uelewa wetu una adhari kubwa katika maisha yetu. Kwa vyote hivyo vinatusaidia kufanya maamuzi, na kila siku mwanadamu hufanya maamuzi. Kufanya maamuzi hupelekea kubadili maisha yetu kabisa. Kila siku kuna maamuzi mbalimbali unayoamua mfano aina ya chakula cha kula, jinsi ya kutumia kipato, watu wa kuongea nao, nini cha kuongea nao na kadhalika na vyote hivi hubadili sehemu fulani katika maisha yetu.
 
c010c81e1ea92ad56d9736ea9209b494.jpg
[emoji91] [emoji91] [emoji91] [emoji91] [emoji91] [emoji91] [emoji91] [emoji91]
Season 6?
 
Zifuatazo ni imani zinazoweza kukurudisha nyuma katika kufikia malengo yako:

+Imani ya kuona ni Vigumu sana kutimiza malengo yako,
Unaweza ukawa na malengo yako lakini ndani yako kuna imani ya kuamini kuwa malengo yako ni vigumu sana kuyatimiza. Kama unafikiri malengo yako ni vigumu sana kutimiza jiulize, ni njia gani ndogo ndogo zinazoweza kukusaidia taaratibu kutimiza malengo yako?
 
Tambua kuwa maisha yanaweza kubadilika katika sekunde moja na kubadili maisha yako kwa ujumla. Fikiria mwaka jana siku kama hii na muda kama huu ulikwepo wapi? Je ulitegemea ungefika hapa? Je ulitegemea leo hii ungekuwa hivi? Fikiria miaka 10 au 5 iliyopita bado utaona kuwa maisha yanabadilika sana. Hakuna kilicho kigumu bali ugumu upo kwenye imani yako. Fanya unachokipenda hata kama kwa dakika tano tu kilasiku kifanye.
 
Back
Top Bottom