Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mashirika mawili ya reli yanayohudumia Tanzania: ni TRC (Shirika ya Reli Tanzania - Tanzania Railways Corporation) na TAZARA (Tanzania-Zambia Railways Corporation). TRC imetawala reli ya kati kuanzia Dar es Salaam hadi Kigoma halafu reli ya Tanga kati ya Tanga na Arusha. Tazara imeunganisha Dar es Salaam na kusini ya nchi hadi Zambia. Zote hazikutunzwa vizuri na usafiri unakumbwa na huduma mbaya pamoja na ajali.
 
c74ced254a14435d834a822a1da62a60.jpg

Emmyta
 
Huduma kwa ndege zatumia hasa viwanja vya ndege 11 vyenye barabara ya lami kwa ajili ya ndege, hasa Julius Nyerere/Dar es Salaam, Kilimanjaro /Arusha-Moshi na Zanzibar-Kisauni. Pia kuna viwanja vingine vya ndege ambavyo ni uwanja wa ndege wa Mwanza, Bukoba na Kigoma.
 
Usafiri wa majini pia unafanyika hasa katika bahari ya Hindi, hakuna meli ya serikali hapo na mashirika binafsi hutoa huduma. Usafiri wa majini hufanyika pia katika maziwa ya Victoria,Tanganyika na Nyasa. Miongoni mwa Meli ni MV Bukoba iliyozama mwaka 1996
 
Katika ziwa Tanganyika ipo meli ya Mv Liemba ambayo ilianza kutumika tangia kipindi cha ukoloni was wajerumani, inatoa huduma kati ya miji ya mwambao wa ziwa Tanganyika na nchi jirani
 
Mwaka 2017 ulianza ujenzi wa awamu ya kwanza ya njia ya geji sanifu nchini Tanzania inayolenga kuunganisha Dar es Salaam na Morogoro[5]. Njia hii inatarajiwa kuendelea hadi Mwanza na hatimaye hadi Burundi.
 
Mwaka 2017 ulianza ujenzi wa awamu ya kwanza ya njia ya geji sanifu nchini Tanzania inayolenga kuunganisha Dar es Salaam na Morogoro[5]. Njia hii inatarajiwa kuendelea hadi Mwanza na hatimaye hadi Burundi.
 
Uchongaji wa mabombwe ya Kimakonde yamesifiwa tangu mwanzo wa karne ya 20. Wamakonde wengi wamehamia Daressalaam au Arusha wanapohudumia soko la watalii na soko la nje.

Tangu miaka ya 1970 uchoraji wa "tingatinga" umejulikana: ulipata jina hilo kutoka kwa Edward Tingatinga naye mtu wa Umakonde.
 
Kati ya wasanii wa Tanzania ni hasa wajume wa ubao na wachoraji waliojulikana kimataifa.

Uchongaji wa mabombwe ya Kimakonde yamesifiwa tangu mwanzo wa karne ya 20. Wamakonde wengi wamehamia Daressalaam au Arusha wanapohudumia soko la watalii na soko la nje.
 
Utamaduni wa Watanzania ni pamoja na utaraab. Muziki ana nyimbo za kitaraab ndizo muhimu sana kwa nchi nzima, hasa visiwani na pwani. Pia kuna miziki ya Kinyarwanda, dansi kama intore n.k.
 
Mahali pafuatapo katika Tanzania pamepokewa katika orodha ya UNESCO ya "Urithi wa Dunia".

(mwaka wa kukubaliwa - jina la mahali)

1979 – Hifadhi ya Taifa Ngorongoro
1981 – Hifadhi ya Serengeti
1981 – Magofu ya Kilwa Kisiwani na Songo Mnara
1982 – Hifadhi ya Taifa Selous
1987 – Hifadhi ya Taifa Kilimanjaro
2000 – Mji Mkongwe wa Jiji la Zanzibar / Unguja
2006 – Michoro ya Kondoa
 
Dar es Salaam ilikuwa ikiitwa “Mzizima”(Ikimaanisha mji wenye neema), ni mji wa zamani ulioanza mwanzoni mwa miaka ya 1857. Ingawa historia ya Mzizima ilianza tangu miaka 1000 iliyopita ambapo watu wa Barawa (ambao walijichanganya na Wazaramo na kuwa kati yao) ambao walitulia na kulima katika maeneo ya mbwa maji magogoni (kwa sasa kivukoni), Mjimwema na Gezaulole.
 
Mji ulianza kuonesha mabadiliko kutokana na ujio wa wa Masultani, Wajerumani na Waingereza. Mwaka 1866 Sultan Seyyed Majid of Zanzibar aliupa jina la ambalo ndilo linalotumika sasa neno la kiarabu lililomaanisha “Mbingu ya Amani”.
 
Baaba ya kifo cha Sultan Majid mwaka 1870, Dar es Salaam ilianguka lakini iliinuka tena mara baada ya ulio wa kampuni ya Kijerumani (German East Africa Company) iliyoanzisha kituo cha biashara mwaka 1887 na kuuondoa utawala wa Kiarabu hata kutawala pwani ya Africa Mashariki.
 
Back
Top Bottom