Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kijana mpole dunia ina mengi
Nakuona unavyo mwangalia sasa nimeipenda njia yako mpya
50feb7f7cccf5f2a2a60e338c7884ae7.jpg
 
Kila mwanadamu anapenda kuwa na furaha, furaha ni lengo la muhimu sana kwenye maisha yetu sisi wanadamu. Kama ilivyo kawaida kwa watu wengi, kila mmoja anapenda kuwa na siku yenye furaha, wiki yenye furaha, mwezi wenye furaha na mwaka wenye furaha. Wanadamu tunaweka sheria mbalimbali za kuishi ili tuishi kwa amani na furaha, tunajituma na biashara na kazi ili tuwe na maisha mazuri yenye furaha. Tunaishi na watu vyema ikiwemo ndugu zetu na wanafamilia ili tuwe na amani na furaha. Kila tunachokifanya katika maisha yetu tunalenga kuwa na furaha.
 
Tukisema tuweze kuchambua sana kuhusiana na jinsi tunavyoitafuta furaha, ni mlolongo mrefu na mifano mingi tunaweza kupata katika kuchambua lengo la furaha na maisha ya wanadamu. Lakini mbali na yote, tunaanza mwaka mpya na ni vyema tukumbuke mambo machache katika kutafuta furaha yetu ya maisha.
 
Weka Fikra na Kipaumbele Ambapo Panakupa Furaha

Kila siku, ni nafasi yetu kuamua kuwa na furaha au kutokuwa na furaha. Katika kila jambo na katika kila hali tunaweza kuchagua kuwa na furaha au kuwa na fikra katika upande mbaya wa hasi. Ukichunguza vizuri katika maisha yetu, bila kujali mtu unapata taabu gani za maisha; lazima utapata kitu ambacho kinakupa furaha. Hakuna mwanadamu ambaye ana taabu kwa asilimia zote.
 
Unapoanza mwaka upya, weka nia ya kuhakikisha kuwa unaweka kipaumbele katika nafasi, watu , hali, vitu au chochote kinachokupa furaha. Acha kushikilia huzuni na majuto bali weka akili yako kwenye furaha. Chukulia mwaka mpya ni nafasi ya kuanza mwaka kwa furaha na chunguza kinachokupa furaha kisha kipe kipaumbele.
 
Weka Urafiki na Upendo Mkubwa Kwako kuliko Mtu Yeyote

Wanadamu wanaweza kukufanya ukakosa furaha, kwa sababu wanadamu hawatabiriki. Lakini wewe mwenyewe unaweza pia kujipenda na kuweza kuwa na amani ya moyo. Kujipenda tunakozungumzia sio kujipenda kwa ubinafsi, bali kwa kujijali, na kujithamini. Jiheshimu na jipe kipaumbele katika maisha yako. Tenda matendo yenye faida kwa mwili wako na afya yako, jiheshimu na hakikisha unajithamini vyema. Hii itakusaidia kuwa na amani hata kama watu wakikupa huzuni, utaendelea kufurahia urafiki ulioweka na nafsi yako binafsi kuliko kuumizwa.
 
Jifunze kuwa na Furaha Hata Katika Nyakati Zenye Shida.

Kama nilivyosema hapo awali, katika kila hali tunayokutana nayo, kuna upande hasi na upande chanya. Ni sisi wanadamu ndio tunakuwa na maamuzi ya kuchagua ni upande upi tuupe kipaumbele zaidi ya upande mwingine. Tazama pande zote na kisha jifunze kupitia matokeo yote na usiruhusu kupoteza amani na furaha yako ya moyo.
 
Wapo wanadamu walioweza kujitambua na kuamka katika maisha. Wengine ni viongozi wa imani kuu duniani, ni walimu wa imani, walimu wa maisha, mifano ya kuigwa lakini wote hawa wanatufundisha kuwa mwanadamu ana uwezo zaidi ya alio nao.
 
Ni vigumu sana kukuambia kuamka ni nini. Maana kuamka ni hali ya kufahamu uhalisia wa ulimwengu, kuungana na chanzo kikuu cha ufahamu, na kujitambua. Ni vigumu kumwambia mtu experience yake ilivyo kwani experience haielezewi bali unatakiwa uiexperience na sio kuisikia. Ni sawa na mtu akikuelezea Los Angeles ilivyo wakati wewe hujawahi kufika. Utajikuta unatengeneza picha ndani ya akili yako, na huenda ukawa unatengeneza picha tofauti kabisa na uhalisia. Ni sawa na kumuelezea kipofu rangi nyekundu ni nini wakati hajawahi kuona rangi.
 
Back
Top Bottom