Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uharibifu kwa mfumo mkuu wa neva na mfumo wa neva za pembeni unaweza kusababishwa matumizi kila mara ya pombe.[2][3] Matumizi ya pombe kupita kiasi kwa muda mrefu yanaweza kuharibu takribani kila kiungo na mfumo katika mwili.[4] Ubongo unaokua wa kijana aliyebaleghe huwa hasa katika hatari kubwa ya kudhurika na sumu ya pombe.[5]
 
Kihistoria, madaktari wametetea pombe kwa faida zake za kiafya na hivi karibuni kwa ajili ya uwezo wake wa kulinda watumiaji dhidi ya ugonjwa wa moyo. Kuna ushahidi wa faida kwa mishipa ya moyo inayotokana na kutumia kinywaji 1- 2 kwa siku, hata hivyo, faida za kiafya kutokana na unywaji pombe kwa wastani ni swala lenye utata.
 
Shauku zimetolewa kuwa sawa na ilivyo katika sekta ya dawa, wadau wa sekta ya pombe piawamehusika katika kutilia chumvi faida za kiafya za pombe. Pombe inapaswa kuonekana kama dawa ya burudani yenye uwezo mkubwa wa kusababisha athari mbaya kwa afya na hipependekezwi kwa-ulinzi wa moyo badala ya mbinu nyinginezo za salama na zilizothibitika za jadi kama vile lishe bora mazoezi na tiba za dawa.[6][7]
 
Baadhi ya wataalamu wanadai kuwa faida za matumizi ya pombe ya wastani zinaweza kupitwa na ongezeko la hatari ikiwa ni pamoja na majeraha, vurugu, uharibifu wa mimba, aina fulani za saratani, ugonjwa wa kongosho na presha.[8] Kwa vile faida bainifu za kiafya za matumizi ya pombe ya wastani ni ndogo kwa watu walio katika hatari ndogo ya kupata maradhi ya moyo,
 
wataalamu wengine wanatahadharisha itumike kwatahadhari kwa sababu ya uwezekano kwamba kupendekeza matumizi wastani ya pombe kunaweza kusababisha ongezeko la hatari ya matumizi mabaya ya pombe, hasa miongoni mwa vijana.[9] Manufaa haya ya matumizi wastani ya pombe yanapitwa na hatari za matumizi ya pombe wastani.[8]
 
Madhara mabaya ya matumizi ya pombe kwa muda mrefu kupita kiasi ni sawa na yale yanaoonekana katika vitulizi-hipnoti vingine (mbali na sumu kwa viungo ambayo hutatiza zaidi katika pombe). Athari za kujiondoakatika pombe na utegemezi hukaribia sana kufanana.[10] Pombe cha kiwango wastani ina athari chanya na hasi kwa afya.
 
Matumizi sugu na mabaya ya pombe huwa na athari kubwa kwa afya ya mwili na akili. Unywaji sugu wa pombe kupita kiasi au utegemezi pombe, unaweza kusababisha uharibifu mpana viungo mbalimbali vya nevaza ubongo,mfumo wa neva ama ugonjwa wa mishipa ya moyo, maradhi ya ini, na neoplasmsi isiyopona.
 
Matatizo ya akili ambayo huhusishwa na ulevi ni pamoja na mfadhaiko mkubwa, disthimia, mania, hipomania, tatizo la hofu fobia , tatizo la wasiwasi wa kijumla, tatizo la tabia za mtu, skizofrenia, kujinyonga, upunufu wa mfumo wa utendakazi mwilini (km kazi za kumbukumbu, hisia, kazi za uamuzi, uwezo wa kuona,mwendo na uwiano) na uharibifu wa ubongo.
 
utegemezi wa pombe ni huhusishwa na shinikizo la damu, ugonjwa wa moyo na kiharusi cha iskemi, kansa ya mfumo wa upumuaji, mbali pia na saratani ya mfumo wa mlo, ini, kifua na ovari. Unywaji kupita kiasi huhusishwa na ugonjwa wa ini, kama vile sairosi.[
 
Utafiti zimelenga wanaume na wanawake, vikundi vya umri mbalimbali na watu wa makundi mengi ya kijamii. Machapisho kwa sasa yanafikia jumla ya mamia huku tafiti zikiweza kuonyesha uwiano uliopo kati ya matumizi wastani ya pombe na afya ambayo labda yanaweza kuwa yalitokana na athari za manufaa ya maingiliano ya kijamii ambayo mara nyingi huambatana na matumizi ya pombe. Baadhi ya njia mahususi ambapo pombe huweza kuathiri afya ya mishipa ya moyo zimetafitiwa
 
Utafiti fulani katika baadhi ya nchi umedai kuwa vifo vinavyosababishwa na sababu zozote zile vinaweza kufikia viwango vya baina ya 16 hadi 28% kwa uchache miongoni mwa wanywaji wa wastani (vinywaji 1-2 kwa siku) ikilinganishwa na ile miongoni mwa wanaojiepusha na unywaji kabisa.[14][15][16][17] Mmwandishi wa habari Roni Caryn Rabin wa New York Times anasema kwamba takwimu za utafiti huu zina makosa.[
 
Nchi mbalimbali hupendekeza kiasi tofauti cha upeo wa kunywewa . Kwa nchi nyingi kiasi cha upeo kwa wanaume ni 210g-140g kwa wiki. Kwa wanawake, kiasi ni 84g-140g kwa wiki. Nchi nyingi hupendekeza kutumiwa kwa pombe kabisa wakati ujauzito ama kunyonyesha.
 
Matumizi ya pombe kupita kiasi ni mojawapo ya sababu zinazoweza kuzuilikaambayo husababisha vifo vingi kote duniani.[19] Utafiti mmoja unahusisha pombe na kila kifo 1 katika 25 kote duniani na kwamba 5% ya miaka wanayoishi watu na ulemavu hutokana na matumizi ya pombe
 
Nchi hukusanya takwimu kuhusu wanaofariki kwa ajili ya pombe. Huku baadhi ya takwimu zikihusiana na athari za muda mfupi kama vile ajali, nyingi huhusiana na athari za muda mrefu wa kutumia pombe.
 
Matatizo ya akili na tabia kutokana na matumizi ya pombe - ICD-10 F10
Kuzorota kwa mfumo wa neva kutokana na pombe - ICD-10 G31.2
Polineuropathi ya pombe - ICD-10 G62.1
Kadiomiopathi ya pombe - ICD-10 I42.6
Gastriti ya Pombe - ICD-10 K29.2
Ugonjwa wa ini wa pombe - ICD-10 K70
Hepatitis sugu , isiyoainishwa mahali kwingine kokote - ICD-10 K73
 
Fibrosi na sairosi ya ini - ICD-10 K74 (bila kujumuisha K74.5 K74.3-Sairosi ya biliari)
Ugonjwa sugu wa kongosho kutokana na pombe - ICD-10 K86.0
Sumu itumikayo kiajali kutokana na mkumbano na pombe - ICD-10 X45
Sumu itumikayo na mtu binafsi kimaksudi kutokana na mkumbano na pombe - ICD-10 X65
 
Back
Top Bottom