3. Kutenda jambo hilo.
Mara baada ya kupata elimu, hamasa jambo linalofuata ni kutenda jambo hilo. Mara nyingi watu wengi huwa wanapata elimu na hamasa tu, jambo ambalo linafanya watu hao waweze kukomea kwenye hatua hizo mbili tu. Ila kwa kuwa wewe ni msaka mafanikio na unataka kufanikiwa zaidi ni vyema ukahakiisha ya kwamba unafika mpaka hatua ya tatu ya kulitenda jambo hilo, na katika kulitenda jambo hilo ni hakikisha unalitenda kwa juhudi zote ulizonazo.