Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mungu hufanya kazi kwa majira na nyakati. Hivyo ni vema utambue majira yako ya kuinuliwa/kubarikiwa mapema ili uone kusudi lako duniani likitimia. Usipoteze nguvu na muda wako kufanya mambo yasiyokuongezea chochote kwenye maisha yako. - - Kumbuka kuna siku zinakuja ambazo hutaweza kukimbia kama unavyokimbia sasa. Wakati una nguvu fanya vitu vitakavyokusaidia wakati huna nguvu. Huu muda unaopoteza kufuatilia maisha ya watu; mara fulani kala hiki; mara huyu na yule wamegombana; mara huyu kasema hiki; mara yule kafanya hivi utaujutia baadae kama hutautendea haki sasa. - - Kumbuka hata yule bibi au babu unayemuona mtaani kwenu alikuwa kijana kama wewe na hivyo alivyo leo ni matokeo ya kile alichokifanya jana.
 
Kuna mahusiano mengine hayaendi hata mlazimishe namna gani, mnajaribu kuweka sawa, kuchumbiana lakini bado ni ugomvi na kukosa furaha...mahusiano ya namna hii wakati mwingine Mungu anakupa ishara kwambia ondoka hapo! Lkn bado umeganda... - - Utagundua baadae ushapoteza muda wako.. Labda baada ya miaka minane katika kubembelezana..... Mtu sahihi mambo yanasonga tu.. Madhaifu au majaribu mengine ni kuchukuliana na kuelewana.
 
MATUKIO : Polisi katika wilaya ya Mpigi wamemkamata mzee moja mwenye umri wa miaka 69 anaanyejulikana kwa jina la Vicent Ssenonga, ambaye ni mganga wa kienyeji kwa kumpa ujauzito binti yake wa kumzaa mwenyewe. Kwa mujibu wa polisi wa kituo cha Buwama ambako mzee huyo anazuiliwa, wamesema walipata taarifa kutoka kwa wasamaria wema kuwa mzee huyo anamnyanyasa binti yake huyo ambaye amemgeuza mke wake, aliyeanza kufanya naye ngono tangu akiwa na miaka 13 mpaka sasa ana miaka 20, huku wakiwa wamezaa watoto watatu. “Kumuoa na kumtesa mtoto wake mwenyewe, kiasi kwamba hampi chakula na huduma za afya, hatukuweza kuvumilia na kwenda kumchukua huyu mzee. Tumeambiwa kuwa amemtumia huyu binti kwa miaka 7 sasa tangu akiwa na miaka 13, na tunachunguza taarifa kuwa amemuambukiza HIV”, amesema Bwana Jospeh Kakama ambaye ni polis wa zamu wa kituoni hapo.
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuhukumu kifungo cha miaka 81 jela mfanyabiashara Timotheo Wandiba baada ya kutiwa hatiani katika mashtaka 27 ya kujipatia Sh2.1 bilioni kwa njia ya udanganyifu.

Mbali ya Wandiba, mahakama hiyo imewaachia huru washtakiwa wenzake wawili; Dickson Okololo na Simon Efrem ambao upande wa mashtaka ulishindwa kuthibitisha mashtaka dhidi yao pasipo kuacha shaka.
 
Akisoma hukumu hiyo jana Machi 13, 2018 iliyoandikwa na Hakimu Joyce Minde, Hakimu Mkazi Mkuu Wilbard Mashauri amesema washtakiwa walikuwa wakikabiliwa na makosa 82 ambapo upande wa mashtaka uliita mashahidi 14.

Katika makosa hayo 82, mashtaka 27 ni ya kughushi, 27 ya kutoa hati za uongo, 27 ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na moja la utakatishaji fedha.
 
Hakimu Mashauri amesema mahakama hiyo imemtia hatiani Wandiba katika makosa 27 ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu baada ya kuridhishwa na ushahidi uliotolewa na mashahidi wa upande wa mashtaka.

Katika makosa hayo, Mashauri amesema katika kila kosa Wandiba atatumikia kifungo cha miaka 3 jela ambapo jumla itakuwa ni miaka 81, lakini kwa kuwa vifungo hivyo vitakwenda sambamba atatumikia kifungo cha miaka mitatu jela.
 
Pia, hakimu amesema mahakama hiyo imemuachia huru Wandiba na wenzake, Okololo na Efrem katika makosa mengine yote baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuyathibitisha pasipo kuacha shaka.

Katika kesi hiyo washtakiwa walikuwa wakikabiliwa na makosa 82 ikiwemo kughushi, utakatishaji fedha na uwasilishaji wa nyaraka za uongo.
 
Wakati kesi hiyo ikiendeshwa washtakiwa walikuwa rumande kutokana na kukabiliwa na shtaka la kutakatisha fedha ambapo kwa mujibu wa sheria halina dhamana.
 
Manchester United wametupwa nje ya michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya hatua ya 16 bora baada ya kuonyesha kiwango kibovu mbele ya Sevilla na kukubali kichapo cha 2-1 Old Trafford.
Wissam Ben Yedder aliyetokea benchi kwa upande wa Sevilla ndiye aliyepeleka kilio kwa Man u baada ya kufunga magoli yote mawili dakika mbili tu baada ya kuingia uwanjani.
Kipindi cha kwanza Man U ilikosa kuongoza baada ya mikwaju ya Marouane Fellaini na Jesse Lingard kuchezwa vyema na mlinda mlango wa Sevilla Sergio Rico aliyeonyesha kiwango bora kwenye mchezo huo.
 
Romelu Lukaku alifunga kwa upande wa United zikiwa zimesalia dakika saba lakini goli lake halikusaidia kitu.
United inaungana na Tottenham kuyaaga mashindano hayo lakini kinara wa EPL Manchester City na Liverpool tiyari wamefuzu hatua ya robo fainali na sasa wanasubiria kupangwa kwa droo siku ya Ijumaa.
Chelsea wanaweza kuungana nao iwapo wataiondosha Barcelona siku ya Jumatano.
 
Meneja wa klabu ya Manchester United Jose Mourinho amesema hatua ya klabu hiyo kutupwa nje ya michuano ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya katika hatua ya 16 bora "si jambo geni" kwa klabu hiyo na si mwisho wa dunia.
Manchester United walilazwa 2-1 na Sevilla uwanjani Old Trafford, mabao yote ya klabu hiyo ya Uhispania yakifungwa na nguvu mpya Wissam Ben Yedder.
"Sifikirii uchezaji wetu ulikuwa mbaya," alisema Mourinho baada ya mechi hiyo ambayo ilikuwa mara ya nne kwake kushindwa katika hatua hiyo ya muondoano Ulaya.
Aliongeza: "Sina majuto. Nilifanya kazi kadiri ya uwezo wangu, wachezaji walijitolea pia. Tulijaribu sana, tulishindwa na hiyo ndiyo kawaida ya mchezo huu wa soka."
United walionekana kuzidiwa na klabu hiyo ya Uhispania mechi zote mbili na Mourinho aliadhibiwa kutokana na timu yake kuwa na tahadhari zaidi katika mechi hiyo ya marudiano Jumanne.
 
United walipoteza nafasi ya kujiunga na wapinzani wao wa jiji Manchester City na Liverpool ambao tayari wamefuzu kwa robo fainali Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.
Mashetani hao wekundu sasa wameshinda mechi moja pekee kati ya tisa walizocheza hatua ya muondoano katika mashindano ya Ulaya na wametolewa kwenye Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya katika hatua sawa katika misimu miwili kati ya mitatu waliyocheza karibuni, awali ikiwa 2012-13 na 2017-18.
United walikuwa wameanza kwa matumaini ambapo katika dakika tano za kwanza Romelu Lukaku alipata fursa ya kumfanyisha kipa wa Sevilla kazi ya ziada, lakini walianza kuzidiwa nguvu baada ya hapo.
Mourinho alisema: "Niliketi kwenye kiti hiki mara mbili katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya baada ya kuwaondoa Manchester United [katiak hatua ya 16 bora] wakiwa kwao nyumbani, Old Trafford. Katika kiti hiki nikiwa na Porto (mwaka 2004) na Real Madrid (mwaka 2013), waliondolewa mara zote mbili. Si jambo geni kwa klabu hii.
"Sifikirii uchezaji wetu ulikuwa mbaya sana, nafikiri nia yetu na jinsi tulivyoanza mechi ilikuwa nzuri na ya matumaini. Sevilla ni timu nzuri na wanaweza kuuficha mpira na wana wachezaji ambao ni wazuri sana katika hilo safu ya kati. Walifanya hivyo kipindi kirefu cha mechi.
"Nafikiri bao la kwanza kawaida lingekuwa muhimu sana, sio tu kwa sababu ya matokeo ya mkondo wa kwanza lakini pia kwa sababu ya umuhimu wa mechi yenyewe.
 
Wakati mwingine huwa nabahatika na mabadiliko ninayoyafanya kwenye kikosi, wakati mwingine unakuta mameneja wengine ndio wanaobahatika. Ilikuwa vyema, na hatua nzuri kwa Vincenzo kumuingiza uwanjani Ben Yedder (aliyefunga bao). Walipofunga bao la kwanza, mechi ilibadilika kabisa."
 
Sevilla ndiyo klabu ya tatu pekee kufunga mabao mawili au zaidi Old Trafford dhidi ya United uchini ya ukufunzi wa Mourinho (Manchester City mara mbili na Burnley).
City ndiyo klabu nyingine pekee iliyofanikiwa kuwalaza United Old Trafford chini ya Mourinho (1-2 Septemba 2016 na 1-2 Desemba 2017).
Ikizingatiwa kwamba Manchester City wanaelekea kushinda Ligi ya Premia, United sasa wataangazia Kombe la FA katika tumaini lao la pekee kushinda kikombe msimu huu.
Watakutana na Brighton katika raundi ya sita Jumamosi.
 
TUTHAMINI UTU NA HESHIMA KWA MKUBWA NA MDOGO TUSIISHI KWA MAZOEA:
Wewe Umeenda semina Dodoma, una ndugu yako kule. Unamtaarifu unakuja kumtembelea. Anakuambia karibu sana. Anakuelekeza panda daladala za Chamwino shukia st Gaspar. Unashuka stendi unamkuta ndugu yako na mkewe na watoto stendi wamekuja kukupokea! Mnatembea kitambo na kufika kwake. Watoto waliobaki home wanakuja ulipokaa, wanakushika kichwani kukusalimia. Wakubwa kidogo wanakuja wanapiga magoti "shikamoo baba mkubwa!".
Wanakuzunguka kuulizia habari za ndugu zao unawasimulia, huyu std 2, huyu std 7, kaka yenu form 2. Ndani kumechangamka kila mtu yuko engaged nawe in one way or another.
Mama anahangaika na msichana kukuandalia chakula. Shemeji yako anakuja kupiga magoti kukuambia karibu chakula. Unaenda mezani anakuja kukunawisha na maneno "tusamehe shemeji mboga zenyewe hivyo hivyo...".
Baadaye unaaga. Nyumba nzima wanafunga, wanakusindikiza hadi kituoni. Watoto wanakuaga, "ba mkubwa msalimie Jerry a Irene. Ukijabtena uje nao!
Unaondoka kwa heshima zote (bila wewe kuonja kiviile!)

Siku ya siku nduguyo naye kapata kitrip cha Dar. Anakuambia nakuja kukutembelea. Unamwambia tumehamia kwetu mbezi panda mwendokasi hadi mbezi mwisho. Anafika anakupigia, unasema kuna bodaboda hapo mpe niongee naye. Unaongea na boda "huyo jamaa mlete kwangu geti linatazamana na kituo cha afya cha mbezi, lina waya za umeme juu". Anafkishwa. Anagonga kengele, mko ndani familia, unaagiza housegirl, "si mnasikia kengele? Kafungueni geti".
Anaingia sitting room anawakuta. Anawasalim unaitikia marahaba, we mkubwa! Mkeo anaangalia tamthilia kakaa chini. Anageuka, karibu shemeji, za siku! "Nzuri". Amemaliza, anaendelea na tamthilia.
Madogo wanacheza computer game hata hawajashituka kuna mtu kaingia. Unasema, nyie msalimieni baba yenu mdoo. Wanatupia shikamoo bila hata kumuangalia usoni, game limekolea!
Mnachati kigogo, unaanza kuchat, mama naye ana mchezo na anachat! Maisha ni ya wote kujaa sitting room, lakini kila mtu kama hayupo vile. Mara housegirl anawakaribisha chakula. Mama anapokea "shemeji karibuni chakula".
Baba unasema "we jitegemee, hapa kima mtu anakula kwa wakati wake!". Mgeni anainuka kwenda kupambana na meza kupakua. Maji ya kunawa hakuna! Bahati hg anakatiza, anaulizwa maji yakunawa, anajibu kanawe pale kwenye hw basin maji yanatoka!

Anakula peke yake, anamliza na kurudi sitting. Mnaongea issues kidogo za kifamilia na wazazi kijijini. Muda unafika wa ndugu kuaga. Unamwambia subiri kidogo. Unapiga kwa boda boda. Anakuja, unatoa elfu kumi unamwambia pata na we nauli. Boda inakuja, anaaga, unasimama unamtoa hadi mlangoni. Wanafamilia wengine wanaagia sitting room bila kuinuka.
Ndugu anakamata mchuma na kuondoka.
TUBADILIKENI JAMANI
 
Mwanafizikia Stephen Hawking Afariki Dunia



Prof Stephen Hawking, mwanafizikia maarufu duniani, amefariki dunia akiwa na miaka 76, familia yake imetangaza.

Mwingereza huyo alifahamika sana kwa kazi yake ya kisayansi kuhusu uwepo wa eneo katika anga za juu ambapo nguvu za mvutano huwa za juu sana kiasi kwamba miali nururishi au hata mwanga hauwezi kuponyoka.

Kwa Kiingereza, eneo hilo hufahamika kama 'Black Hole', Alitumia hilo katika kujaribu kufafanua kuhusu asili ya vitu vyote duniani na angani.

Alikuwa mwandishi wa vitabu kadha maarufu vya sayansi kikiwemo A Brief History of Time (Historia Fupi kuhusu Wakati).

Watoto wake, Lucy, Robert na Tim, wamesema: "Tumehuzunishwa sana kwamba baba yetu mpendwa ametuacha."

"Alikuwa mwanasayansi muhimu na mtu wa kipekee ambaye kazi zake na mchango wake vitaendelea kukumbukwa kwa miaka mingi."



Alizaliwa 8 Januari 1942 Oxford, EnglandAlipata nafasi chuo kikuu cha Oxford kusomea sayansi ya mambo asilinia mwaka 1959, kabla ya kwenda kusomea shahada ya uzamifu chuo kikuu cha CambridgeKufikia 1963, alipatikana na ugonjwa ulioathiri mfumo wake wa neva na mawasiliano mwilini. Madaktari walimwambia hangeishi zaidi ya miaka miwili.Alieleza nadharia yake kwamba 'black hole' kutoa "Miali ya Hawking" mwaka 1974Alichapisha kitabu chake A Brief History of Time mwaka 1988. Nakala zaidi ya 10 milioni za kitabu hicho ziliuzwa.Maisha yake yaliangaziwa kwenye filamu ya The Theory of Everything ya mwaka 2014 ambapo Eddie Redmayne aliigiza nafasi ya mwanasayansi huyo
Stephen Hawking alipokuwa na miaka 22 pekee aliambiwa na madaktari angeishi miaka mingine miwili pekee baada yake kupatikana na ugonjwa nadra sana wa mfumo wa neva.

Ugonjwa huo ulimfanya kulemaa na kulazimika kutumia kiti cha magurudumu.

Nyakati za mwisho za maisha yake, alikuwa hawezi kuzungumza ila kwa kutumia kifaa cha kufasiri mawazo yake na kuyageuza kuwa sauti.
Rip
 
B47EC196-144A-4D11-AB39-8DE3FACDF698.jpeg
 
Back
Top Bottom