Mimi sijawahi kupanda treni hata siku moja, kumbe iko hivi nashukuru sana,” amesema Mwanaisha Isasa mkazi wa Chang’ombe mjini Dodoma.
Uzinduzi huo umehudhuriwa pia na wabunge na viongozi mbalimbali wa chama na Serikali.
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Rahco, Masanja Kadogosa amesema mkataba wa ujenzi wa reli ya kisasa kati ya Morogoro na Dodoma ulisainiwa Septemba 29, mwaka jana kati ya Kampuni ya Rahco na Yapi Merkezi Inssar Sanay’s ya Uturuki.
Treni hiyo ya mwendokasi itakuwa ikisafiri umbali wa kilomita 160 kwa saa itajengwa kwa gharama ya dola 3.457 za Marekani.