Jose Mourinho amebakiza nafasi moja tu ya kujifariji msimu huu ni kutwaa ubingwa wa Kombe la FA.
Mourinho na uwekezaji wake wote aliofanya kwenye kikosi chake cha Manchester United, amevuruga kwenye michuano yote iliyoshiriki timu yake msimu huu na kubakiza Kombe la FA tu, ambapo hii leo, Jumamosi atafahamu hatima yake huko Old Trafford atakapowakabili Brighton katika robo fainali ya michuano hiyo.
Habari mbaya kuhusu michuano hiyo ni kwamba Tottenham Hotspur, Chelsea na Leicester City bado hawajatoka, hivyo kwa uchezezaji wa timu hiyo ya Mourinho kwa msimu huu, chochote kinaweza kutokea.