Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Meneja wa Chelsea Antonio Conte amesema mlinzi wa kati Gary Cahill na mshambuliaji Alvaro Morata wanahitaji juhudi zaidi iwapo wanataka kurejea katika kikosi cha kwanza na kuweka uwezekano wa kuziwakilisha timu zao za taifa ambazo ni Uingereza na Hispania.(Express)

445520388_223817.jpg
 
Conte anaamini hawezi ondolewa kwenye klabu ya Chelsea iwapo mabingwa hao wa msimu uliopita hawatafuzu kucheza klabu bingwa ulaya msimu ujao.(Telegraph)
 
Mtandao maarufu wa Facebook umetangaza kusimamishwa kwa akaunti ya Strategic Communication Laboratories kampuni mama ya Cambridge Analytica, kampuni ya uchambuzi wa data inayotuhumiwa kuratibu kampeni za mgawanyiko kuelekea uchaguzi mkuu wa rais mwaka 2017 nchini
 
Facebook imedai kwamba mnamo mwaka 2015 Cambridge Analytica ilipewa maelezo jinsi ya kutumia Facebook bila idhini kutoka mtandao huo kupitia kazi iliyofanywa kwa ushirikiano na Profesa wa Saikolojia ya Chuo Kikuu cha Cambridge aitwaye Dr Aleksandr Kogan.
 
Profesa huyo alisema uongo na kukiuka sera zetu za jukwaa kwa kupitisha data kutoka kwenye programu ambayo ilikuwa ikitumia kuingia FB kwenda SCL / Cambridge Analytica, ambayo inafanya kazi za kisiasa, serikali na za kijeshi kote ulimwenguni. Pia alimpatia data Christopher Wyloe wa kampuni ya Teknolojia ya Eunoia," ilisema Facebook.
 
Ripoti iliyotolewa mwaka jana na kampuni ya kimataifa ya masuala ya faragha yenye makao yake London, Uingereza, inayopigana haki ya faragha duniani, ilisema kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2017, kampuni ya Cambridge Analytica iliongoza kampeni za mtandao ambazo zililenga ama kumshambulia kiongozi wa Nasa Raila Odinga au kumpigia debe Rais Kenyatta.
 
Facebook ilisema kuwa kampuni hiyo kipekee ilimfanyia kazi Rais Kenyatta wakati wa kampeni yake ya uchaguzi.

Cambridge Analytica ilikanusha madai na ikasema kuwa haikuhusika katika maudhui yoyote hasi ya kisiasa.
 
Muheza.Watahiniwa wa kidato cha sita katika shule ya “New Age open”ya jijini Tanga,jana Machi 16, walitoa msaada wa vyakula,sabuni,nyavu za mbu na simu kwa wazee walioathirika na ukoma wa kituo cha Misufini Wilayani hapa ili kupata baraka zao kabla ya kufanya mtihani wa kitaifa Mei mwaka huu.
 
Watahiniwa hao 29 wamefanya hivyo wakifuata nyayo za watangukizi wao 35 waliofanya mitihani kama hiyo mwaka jana waliopeleka msaada kama huo na kujikuta wakipata ufaulu wa kuwawezesha wote kupata mkopo wa Serikali katika vyuo vikuu walivyochaguliwa.
 
Wakizungumza wakati wakikabidhi msaada huo watahiniwa hao wamesema licha ya kwamba walimu wao wamefanya kazi ya ziada kuwafundisha itakayohakikisha wanafanya vyema mitihani ya kujiunga na elimu ya juu lakini baraka za wazee hao waathirika wa ukoma zina umuhimu wa aina yake.
 
Tumekuja hapa tukiamini kwamba wakifurahi wazee hawa kwa ajili yetu watatupa baraka za kutuwezesha kufanya vyema mitihani ya Taifa ya kidato cha sita na kwenda vyuo vikuu wote”amesema Shedrack Mnzava ambaye ni kiongozi wa wanafunzi hao wa kidato cha sita.
 
Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro limekiri kumhoji Mkuu wa pili wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi Kilimanjaro Kati, Mchungaji Fred Njama.

Hatua ya polisi kumkamata na kumhoji Mchungaji Njama inakuja ikiwa zimepita siku chache tangu kiongozi huyo wa kiroho kutaja mambo sita aliyodai yanaitafuna nchi
 
Akizungumza na Mwananchi leo Machi 17, 2018, Kamanda wa Polisi Mkoa huo, Hamis Issah amesema; “suala hilo limeshughulikiwa na kamati ya ulinzi ya wilaya na mimi bado halijanifikia ili niwe na nafasi nzuri ya kulizungumzia.”

Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Kippi Warioba amesema; “suala hilo siwezi kulizungumza katika simu.” Huku akimtaka mwandishi kufika ofisini kwake na atalizungumzia.
 
Back
Top Bottom