Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Labda hii watanzania wengi wangedhani ndio inayoongoza maana ndio tumejikita huku lakini ukweli ni kuwa inashikilia namba nane.Watu wanapenda kujipiga picha sana basi Instagram ndio penyewe katika kupost vitu vya namna hiyo.
 
#10 Yahoo Stocks



Duniani sasa hivi wengi wanapenda kuwekeza kwenye masoko ya hisa.Tofauti na miaka ya nyuma ambapo si wengi wa rika la ujana walipendezwa na biashara hii sasa hivi hata vijana wanajihusisha na uwekezaji wa aina hii.Basi apps hii imachukua nafasi kuliko unavyoweza kudhani.
 
HISTORIA: Inadaiwa kuwa vita fupi zaidi kuwahi kupiganwa duniani ni kati ya Zanzibar dhidi ya England mnamo mwaka 1896 ambapo vikosi vya utawala wa Zanzibar wakati huo vilikubali kushindwa ndani ya Dakika 38 baada ya vita kuanza.
 
KISTAAJABU ya Firauni utayaona ya Musa, ngoma ambayo imevunja rekodi duniani kwa sasa kuwahi kutengenezwa.

Wazo na muundo wa ngoma waliutoa vijana wawili Brian Fleming wakishirikiana na mwenzake aliyefahamika kwa jina Paraic Breathnac. Hii ilikuwa nchini Ireland na ikapewa jina la “THE IRELAND MILLENIUM DRUM”. Ilikuja kutengeneza na Bill Wright na Seamus Purcell. Ngoma hiyo ina kimo cha futi 6 na inchi 3 na kipenyo ni futi 15 na inchi 6. Ngoma hiyo ilitengenezwa kwa malighafi ya mbao na kitambaa murua kabisa Ngoma hiyo baada ya kutengenezwa ilitumika katika Tamasha moja Machi 13, 1999 lililokwenda kwa jina la Patrick’s Festival Jijini Dublin.
 
najua zawadi ni kitu muhimu sana, sasa sikiliza hii. Zawadi kubwa kuwahi kutolewa katika karne ya 19 ni ile ya zawadi ya Sanamu ya Uhuru ya nchini Marekani. Sanamu hiyo ikapewa jina la Liberty Enlightening the World”.

Zawadi hii ilitolewa na Ufaransa kwa Marekani. Aliyeitengeneza sanamu hii ambayo ilimalizika mwaka 1886 alikuwa ni Auguste Bartholdi akiwa Mhandisi wake Gustave Eiffel.

Ima urefu wa futi 151 na inchi 1 sawa na mita 46 sentimeta 50, usito wake ni tani 225.
 
Burudani ni kitu cha maana sana; lakini kwa hili kiboko kweli kweli maana mmmh!

Ukumbi mdogo zaidi ulimwenguni wa klabu hapa ulimwenguni ni ule wa The Miniscule of Sound uliopo London.

Ukumbi huu una urefu wa futi 8 sawa na meta 2 na sentimenta 4, upana wake ni futi 4 sawa na mita 1 sentimeta 2 na eneo la kuchezea yaani DANCE FLOOR ni mita za mraba 2.
 
Je, unapenda kujipiga picha mnato au selfie mara kwa mara? Watafiti wa Chuo Kikuu cha Nottingham Trent, Uingereza na kile cha Thiagarajar cha India wamebaini kwamba kama unapiga picha zaidi ya tatu kwa siku na kuziweka katika mitandao ya kijamii, basi una dalili za ugonjwa wa akili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…