Licha ya kutokutangazwa na kutambulishwa rasmi, alovera ni moja kati ya mimea itumiwayo kwa kiasi kikubwa duniani. Watu wengi hutambua uwezo wake mkubwa wa kuponya majeraha ya moto na michubuko mbalimbali mwilini. Zaidi ya hili, pia hutumiwa katika matayarisho ya vipodozi na vinywaji mbalimbali. Japokuwa zao hili bado halijakubalika kwa waganga wengi, kuna tafiti nyingi linafanyiwa kila mara kuhusu uwezo wake katika kuponya maradhi mbalimbali.