Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

UGONJWA WA GUMBORO UNAVYOATHIRI KUKU : Ugonjwa wa gumboro (Infectious bursal disease) ulionekana kwa mara ya kwanza nchini Tanzania miaka ya 1980. Na inasemekana jamii ya ndege wote duniani wanawezwa kuathiriwa na ugonjwa huu, ingawa kuku ndiyo waathirika wakubwa.

Ugonjwa huu husababishwa na virusi ambavyo hufahamika kama burnaviridies.
 
UAMBUKIZAJI

Ugonjwa wa gumboro husambazwa zaidi kwa njia ya hewa au chakula na ni ugonjwa ambao husambaa kwa haraka sana mara uingiapo ndani ya banda la kuku.

Na inasemekana virusi vya gumboro vinaweza kubaki ndani ya banda la kuku kwa miezi kadhaa.
 
Kuku kushindwa kutembea na kusimama vizuri
Kukosa hamu ya kula
Kuharisha kinyesi cheupe
Manyoya kutimka au kusimama.
Ugonjwa huu unapoingia ndani ya banda la kuku huanza kuua kuku wachache, na baada ya siku ya 4 vifo huongezeka kwa kiasi kikubwa. Kisha vifo hupungua tena katika siku ya 5 hadi 7, na hatimaye kwisha kabisa mnamo siku ya 10 hivi.
 
UCHUNGUZI BAADA YA KIFO

Rangi nyeusi hujionyesha katika nyama (muscles) za kuku aliyepasuliwa

Kuwepo kwa michirizi yenye rangi nyekundu sehemu za mapaja

Viungo huongezeka ukubwa, kubadilika rangi na kuwa nyeupe. Vilevile huonyesha michirizi yenye rangi ya kahawia.
 
Kinyunguu huongezeka ukubwa na kubadilika rangi ikimaanisha damu imevia. Dalili hii mara nyingi hutokea katika siku ya 3 tangu unapoingia ugonjwa bandani. Katika siku ya 5 kinyunguu huanza kupungua na baadaye katika siku ya 8 hurudi kabisa katika hali yake ya kawaida.
 
MATIBABU

Kama yalivyo magonjwa mengine yaenezwayo na virusi, ugonjwa wa gumboro hauna tiba, bali kuku walioathirika inabidi wapatiwe vitamini na dawa kama vile Amprolium, Vitastress, Antistress, multivit CH, Vitalyte, Doxycol, CTC 20%, CTC 20%, na nyinginezo kwa ajili ya kuwakinga na kutibu maambukizo ya magonjwa ya mengine kama coccidiosis na maradhi yanayosababishwa na bakteria.
 
MATIBABU

Kama yalivyo magonjwa mengine yaenezwayo na virusi, ugonjwa wa gumboro hauna tiba, bali kuku walioathirika inabidi wapatiwe vitamini na dawa kama vile Amprolium, Vitastress, Antistress, multivit CH, Vitalyte, Doxycol, CTC 20%, CTC 20%, na nyinginezo kwa ajili ya kuwakinga na kutibu maambukizo ya magonjwa ya mengine kama coccidiosis na maradhi yanayosababishwa na bakteria.
 
KINGA

Ili kuwakinga kuku na maambukizi ya gumboro ni muhimu wapatiwe chanjo ya ugonjwa huu. Chanjo iwe sahihi na ifanyike wakati muafaka. Kwa kawaida kuku wanaweza kupewa chanjo hii kati ya umri wa siku 4 hadi 14, ingawa chanjo ikitolewa mapema, yaani siku ya 4, inaweza kurudiwa. Zipo chanjo za aina nyingi mathalani ya kunyunyiza machoni, ya kunywa, ya kunyunyiza mwilini, au sindano. Jambo lililo muhimu ni kuzingatia maelekezo kwenye lebo au viambatisho kwenye kasha/chupa ya dawa.
 
Mfugaji anaweza kuondoa uwezekano wa kutokea kwa ugonjwa huu kwa kuwa na banda safi, lenye nafasi kubwa, linaroruhusu hewa na mwanga mwingi. Pia kutumika vyombo visafi, chakula na maji safi, na kuepuka mwingiliano wa kuku wazima na wanaosumbuliwa na magonjwa mengine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…