Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

UZALISHAJI WA ASALI : Asali na nta ni moja ya mazao makuu ya nyuki nchini Tanzania, Tanzania ina mazingira mazuri ya kuzalisha asali kwa kiwango cha juu cha ubora kutokana na kuwepo kwa aina nyingi na spishi za mimea inayozalisha chakula cha nyuki (mbochi na chavua). Kutokana na sababu hizo, asali inaweza kupata soko lenye bei ya juu endapo tutadumisha ubora wake.
 
Asali hutumika kama chakula, dawa na zao la biashara. Aidha, asali hutumika kama kiambato muhimu katika uokaji, viwanda vya vyakula vitamu, vipodozi, vinywaji na viwanda vya dawa. Kwa mujibu wa Sera ya Taifa ya Ufugaji Nyuki ya Machi 1998 na Programu ya Taifa ya Ufugaji Nyuki ya Novemba 2001, Tanzania huzalisha takriban tani 4,860 za asali. Taarifa ya mwaka 2006 ya Idara ya Misitu na Nyuki inaonesha kuwa Tanzania husafirisha nje ya nchi wastani wa tani 500 za asali. Wanunuzi wakuu wa asali ya Tanzania ni nchi za Ujerumani, Uingereza, Uholanzi, Ubeligiji na Uarabuni.
 
Licha ya soko zuri la asali, matakwa ya viwango vya ubora vinavyohitajika kwa ajili ya soko la ndani na nje ya nchi hayajawafikia kikamilifu wafugaji nyuki na wadau wengine. Hali hii husababisha kuzalishwa kwa asali yenye kiwango duni na kusababisha zao hili kuuzwa kwa bei ndogo.
 
ASALI NA MUUNDO WAKE

Asali huundwa kwa sukari na maji. Kwa wastani asali huwa na sukari kiasi cha asilimia 79.6 na maji asilimia 17.2. Kiasi kikubwa cha sukari zinazounda asali ni fruktosi (asilimia 38.2) na glukosi (asilimia 31.3). Hizi ni aina rahisi za sukari ambazo zinaweza kufyonzwa mwilini kwa wepesi zaidi.
 
Aina nyingine za sukari ni pamoja na malitosi (asilimia 7.3) na sukrosi (asilimia 1.3). Asali pia ina asidi (asilimia 0.57), baadhi ya protini (asilimia 0.26), kiasi kidogo cha madini (asilimia 0.17) na viasili vya rangi.
 
Maandalizi ya Mizinga ya Nyuki :

Mizinga itengenezwe kwa malighafi nafuu inayopatikana kirahisi, mbao zilizokauka na ambazo nyuki wanazipenda (pata ushauri kutoka kwa afisa ugani au mfugaji nyuki mzoefu).
 
Vibanda maalum vya nyuki vijengwe ili kuleta kivuli na kulinda makundi ya nyuki katika maeneo ambayo hayana miti ya kutosha kwa ajili ya kivuli cha kukinga mizinga.
 
Mizinga iambikwe chambo kabla ya kuwekwa kwenye manzuki kwa kutumia nta ya nyuki, gundi ya nyuki au chambo chochote kinachoweza kupatikana katika maeneo husika.

Vianzio vya kujengea masega vitokane na nta nyuki.
 
Mizinga ya nyuki iwekwe kwenye manzuki ambako mfugaji nyuki anaweza kufanya ukaguzi wa makundi ya nyuki pamoja na kuvuna mazao ya nyuki kwa urahisi.
 
Uvunaji wa Asali :

Uvunaji wa asali ni vema ufanyike kwa kuzingatia mahali manzuki yalipo. Uvunaji wa mazao ya nyuki kwenye manzuki karibu na makazi ya watu ufanyike wakati wa usiku. Manzuki yaliyoko mbali na makazi ya watu uvunaji ufanyike wakati wowote ili mradi kuna mwanga wa kutosha kumwezesha mvunaji kuona masega kwa urahisi. Tahadhari zichukuliwe ili kuepuka kuchafuliwa kwa asali.
 
Wafugaji wa nyuki wavune masega yaliyoiva tu. Masega mapya yenye asali iliyoiva yatenganishwe na yale ya zamani ili kupata asali yenye rangi moja. Iwapo kwa bahati mbaya masega yasiyoiva yamekatika, mvunaji anapaswa kuyatenga na kuyatumia kwa ajili ya shughuli zingine, kwa mfano, kula au kuwalishia nyuki.
 
Matumizi ya viuatilifu hayaruhusiwi wakati wa kuvuna asali. Pia aina yoyote ya kemikali isichanganywe na viwashia bomba la moshi.

Wavunaji wa mazao ya nyuki watumie vifaa maalum vya kinga wakati wa kuvuna. Kiasi kidogo cha moshi baridi kitumike katika kutuliza nyuki.
 
Vifaa vya kuvunia asali viwe safi, vikavu na vyenye mifuniko isiyopitisha hewa ili kuzuia asali isifyonze unyevu, isiingize uchafu na isichukuliwe na nyuki.

Nyuki lazima waondolewe kwenye masega yanayovunwa.

Masega yenye majana na yenye chavua yasichanganywe na masega yenye asali. Asali iliyochanganywa na majana ni rahisi kuchacha.

Mazao ya nyuki yaliyovunwa yanapaswa kuhifadhiwa mahali penye joto la wastani, pakavu, penye kivuli.
 
Back
Top Bottom