Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Profesa Makame

Mbarawa amewataka watu wanaoishi mabondeni waliogoma kuondoka baada ya

kupata taarifa juu ya hatari inayowanyemelea kuondoka mara moja ili

kuepusha majanga.
 
Mbarawa amesema hivi sasa Mamlaka ya Hali ya

Hewa Nchini (TMA) inatoa taarifa za hali ya hewa inayowataka walioko

katika maeneo ya mabondeni lakini hawako tayari kuondoka.

“Unapopata taarifa ya hali ya hewa kama mahali hapo si lazima maana

yake ni lazima uondoke, vinginevyo utapata shida,”amesema.
 
Amesema lazima kufuata utabiri wa hali ya hewa ili kujiepusha na

majanga yanayoweza kujitokeza kwa kudharau taarifa zinazotolewa na

mamlaka hiyo.

Amesema zingatia taarifa hali ya hewa ndio kaulimbiu ya

maadhimisho yaliyofanyika jana yakilenga watu kutopuuza utabiri

wa hali ya hewa.
 
Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk Agnes Kijazi alisema makubaliano ya kimataifa ni kuwa na utabiri wenye usahihi kwa asilimia isiyopungua asilimia 70.

“Utabiri wetu sasa umeongezeka usahihi tumefika hadi asilimia 88

wakati mwingine tunafika asilimia 90,”amesema.

Aidha, amesema wamekuwa wakishirikiana na taasisi nyingine nchini

katika kuchukua hatua wanapotoa taarifa za kutahadharisha watu.
 
Jeshi la Uhamiaji Mkoa wa Kilimanjaro, limebaini mbinu mpya wanayotumia mawakala kusafirisha wahamiaji haramu ambapo kwa sasa wanawabadili mwonekano kwa kuwanyoa vipara na kuwavisha mavazi yanayotumiwa na kabila la kimasai ili kuvikwepa vyombo vya sheria.

Katika kipindi cha Januari 2017 hadi Machi 22,2018, jeshi hilo limewakamata wahamiaji haramu 208, katika maeneo mbalimbali mkoani Kilimanjaro, kwa tuhuma za kuingia nchini, kinyume cha sheria.
 
Akizungumza ofisini kwake leo Machi 23 Mkuu wa Uhamiaji Kilimanjaro, Naibu Kamishna wa Uhamiaji Albert Rwelamira, amesema Machi 22 mwaka huu, waliwakamata watu wawili katika mpaka wa Holili, akiwemo raia mmoja wa Ethiopia, ambaye alikuwa amevalia mavazi ya kimasai huku akiwa amenyoa upara kwa lengo la kukwepa vyombo vya ulinzi maeneo ya mpakani.
 
Aliwataja watu waliokamatwa kuwa ni Saimon Ngarieni Kalanga (28)Masai, mkazi wa Simanjiro mkoani Manyara, ambaye alikuwa akimsafirisha Kibamo Gashe Abate (26) Raia wa Ethiopia, kwenda nchini Afrika Kusini.

“Katika kupambana na wahamiaji haramu, tuna mitandao tunayoifuatilia, na tumebaini njia wanazozitumia ili kutukwepa kwani awali walikuwa wakipita vichochoroni, lakini kwa sasa wanawabadilisha muonekano, wanawanyoa nywele zote na kubaki upara na kuwavisha mavazi ya

kimasai (rubega) ili kutukwepa,” amesema Rwelamira.
 
Amesema Mtanzania ambaye alikuwa akimsafirisha raia huyo wa Ethiopia, mbali na kumbadilisha muonekano, pia alimbadilisha jina na kumpa majina ya Samuel ili kumficha katika basi walilokuwa

wakisafiria asifahamike kiurahisi.
 
Kwa mujibu wa Kamishna Rwelamira raia huyo wa Ethiopia, alikuwa na hati ya kusafiria namba Ep 50554339, ambayo inaonyesha kutolewa Februari 22 mwaka huu nchini Ethiopia na alitoka nchini humo Machi Mosi mwaka huu akipitia nchini Kenya, ambapo iligongwa muhuri lakini alipofika Tanzania hakuitumia kutokana na utaratibu wa viza uliopo ambao wanadai ni mgumu.
 
Tunaendelea na jitihada za kupambana na mtandao wa kusafirisha wahamiaji haramu ambao unaonekana kuwezeshwa na baadhi ya Watanzania kwani mawakala wa usafirishaji wapo kuanzia Ethiopia kwenyewe Kenya, Tanzania, Zimbabwe hadi Afrika Kusini, na hapa unaweza kuona ni kiasi gani cha fedha wanachotumia katika kazi hii.
 
Pia alisema katika kupambana na hali hiyo tayari wamezungumza na wawakilishi wa kampuni za magari, kuwataka kuwa makini hasa wakati wa ukataji wa tiketi na kuhakikisha wale wanaofika kuwakatia watu

ambao hawapo, wanafika na vitambulisho vyao vyenye picha ili kujiridhisha.
 
Alisema kwa mujibu wa sheria likikamatwa gari lililobeba mhamiaji haramu linatakiwa kutaifishwa hivyo ni vyema wakawa makini na kuhakikisha wanatoa taarifa pindi anapoingia mtu kwenye gari na

kumtilia shaka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…