Amesema baada ya purukushani Ekaterina alifanikiwa kumuangusha mwanaume huyo na ndipo alipopata mwanya wa kufungua dirisha na kuruka nje ambapo Polisi mjini Dubai wameeleza kuwa chumba hicho kilikuwa ghorofa ya sita.
“Tulipigiwa simu na ubalozi wetu (Ubalozi wa Urusi) kuwa mtoto wetu amepata ajali ikabidi tuulize kilichomsibu lakini hatukupewa taarifa kamili hadi tuliposafiri kwenda Dubai,“ameendelea kusema Bi. Inda.
“Kwa bahati nzuri tulimkuta anauwezo wa kuongea lakini alikuwa anashindwa kukaa, alitueleza kilichomsibu kuwa alikimbia mtu aliyekuwa anataka kumbaka, ambaye sisi alitutaarifu kuwa ni rafiki yake kibiashara,“amesema Inda.