Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limewatahadharisha waagizaji wa bidhaa za umeme jua dhidi ya ubora unaokubalika.

Tahadhari hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Uandaaji Viwango wa TBS, Edna Ndumbaro alipokuwa akifungua warsha ya viwango vya bidhaa za umeme jua iliyoandaliwa na shirika hilo kwa kushirikiana na Shirika la Fedha la Kimataifa (IFC).
 
Ndumbaro alisema uwapo wa bidhaa hafifu nchini kunatishia ukuaji wa soko la umeme jua kwani wateja wengi ambao hawataridhika na ubora wake watakosa imani na teknolojia hiyo.

“Ili kuhakikisha bidhaa hafifu zinaondolewa, shirika litaendelea kufanya ukaguzi wa kushtukiza katika maduka mbalimbali. Shirika lina dhamana ya kusimamia uzalishaji wa bidhaa zinazokidhi viwango vya ubora nchini kote, ikihusisha usimamiaji na uandaaji wa viwango.
 
Hii ina maana bidhaa zote za umeme jua au zinazohusiana nao; ziwe zinazalishwa nchini au kuagizwa kutoka nje zinatakiwa kukidhi matakwa ya viwango hivyo,” alisema Ndumbaro.

Mshauri wa masuala ya nishati wa Kampuni ya SNV Tanzania, Felchesini Swai alisema udhibiti huo utasaidia kuongeza bidhaa zenye ubora unaotakiwa nchini.
 
Kuna malalamiko kutoka kwa wasambazaji wa vifaa hivyo kutojua bidhaa zenye ubora. Semina hii itatusaidia kujua bidhaa ipi ni bora,” alisema Swai.

Kampuni nyingi za ndani na kimataifa zinasambaza bidhaa hizo ingawa changamoto inayowakabili wananchi ni kutambua ubora, hivyo kujikuta wakiingia gharama za ziada wanaponunua zisizo na ubora.
 
Waziri wa Afya Zanzibar, Hamad Rashid Mohammed ametoa onyo kwa wafanyabiashara watakaogundulika kuuza dawa zinazotolewa na Serikali bure kwamba watanyang’anywa leseni na kufungiwa biashara zao.

Alitoa onyo hilo katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Kifua Kikuu (TB) Mjini Unguja juzi na kuongeza kuwa hatua hiyo ni moja kati ya juhudi za kusimamia upatikanaji wa huduma za afya kwa kiwango kinachotakiwa.
 
Waziri wa Afya Zanzibar, Hamad Rashid Mohammed ametoa onyo kwa wafanyabiashara watakaogundulika kuuza dawa zinazotolewa na Serikali bure kwamba watanyang’anywa leseni na kufungiwa biashara zao.

Alitoa onyo hilo katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Kifua Kikuu (TB) Mjini Unguja juzi na kuongeza kuwa hatua hiyo ni moja kati ya juhudi za kusimamia upatikanaji wa huduma za afya kwa kiwango kinachotakiwa.
 
Alisema licha ya Serikali kutumia zaidi ya Sh10 bilioni kununua dawa na kuzitoa bure kwa wagonjwa, imegundulika kuwa wapo wafanyabiashara wanaoziuza.

Mohammed alitaja baadhi ya dawa zilizobainika kuuzwa kuwa ni za Malaria na uzazi wa mpango.
 
Pia, alisema Zanzibar imefanikiwa katika mapambano dhidi ya Malaria na kwamba ipo haja ya kuelekeza nguvu kwenye magonjwa.

“Kila kiongozi akiwajibika ipasavyo hakuna uwezekano wa Kifua Kikuu kushambulia wananchi wetu kama ilivyo sasa,” alisema Mohammed.
 
Mfanyabiashara ambaye tutambaini kuhusika na uuzaji wa dawa ambazo sisi hutoa bure kwa wananchi wetu, ajiandae kufungiwa leseni ya kufanya biashara hata awe anauza kidonge kimoja tu cha dawa adhabu hiyo itamkumba tu,” alisema Mohammed.

Akizungumza kuhusu Kifua Kikuu, alisema Serikali imedhamiria kupambana na ugonjwa huo ambao unaonekana kuathiri jamii.
 
Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Dk Andemichel Ghirmay aliiomba Serikali kuongeza juhudi za kutoa elimu kwa wananchi ikiwamo kutambua dalili za Kifua Kikuu na namna ya kujikinga.

Alisema WHO inajivunia kufanya kazi na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) kutokana na ushirikiano wanaoutoa kwa shirika hilo.
 
Meneja wa Kitengo Shirikishi cha Ukimwi, Kifua Kikuu na Ukoma, Farhat Khalid aliiomba Serikali na wananchi kuufanya ugonjwa wa Kifua Kikuu kuwa ajenda ya kudumu katika vikao vyao.
 
Back
Top Bottom