Uzoefu wetu ni kwamba kwa vyombo kama hivi vikubwa huwa ni asilimia 20 ama asilimia 40 yake, ndio hunusurika na kuweza hurudi duniani na kuweza kupatikana ardhini kinadharia," afisa kutoka ofisi ya vifusi vya vyombo vya anga katika shirika la safari za anga za mbali la Ulaya Esa , Holger Krag, amewaambia waandishi wa habari.
"Lakini, kujeruhiwa na moja ya vipande vyake ni jambo ambalo kwa kiwango kikubwa haliwezekani. Makadirio yangu ni kwamba kuangukiwa na chombo hiki ni sawa na uwezekano wa kupigwa na radi mara mbili kwa mwaka."