Numbisa
JF-Expert Member
- Dec 12, 2016
- 348,970
- 1,252,247
Unachopaswa kuelewa kama mtumiaji wa mitandao ya kijamii ni kwamba hakuna usalama kwenye mitandao hii. Mtu yeyote anaweza kujua chochote kuhusu wewe na kutumia taarifa ulizoweka kufanya kile anachotaka. Hivyo kuwa makini ni aina gani ya taarifa unatoa kupitia mitandao hii, na kama hakuna manufaa unayopata kwenye mitandao hii, unaishia tu kuangalia nani kafanya nini, unaweza kuungana na kampeni ya [HASHTAG]#DeleteFacebook[/HASHTAG] na ukapata muda wa kufanya mambo muhimu kwenye maisha yako.