Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Screenshot_2018-03-28-13-07-12.jpg
 
Newcastle imekuwa ikimsaka mchezaji wa kiungo cha kati wa Besiktas Oguzhan Ozyakup, mwenye miaka 24, kwa mtizamo mpya wa kusaini mkataba wa bila malipo na Uturuki katika msimu wa majira ya joto. (Turkish-Football.com).
 
Mshambuliaji wa Aston Villa Gabby Agbonlahor, mwenye umri wa miaka 31, atakamilisha mwaka wake wa 17- wa uhusiano wake na kilabu hicho msimu huu wa majira ya joto, hata kama watapanda na kuingia Ligi ya Primia. (Telegraph)
 
Washiriki wa michuano ya kombe la klabu bingwa wanatarajia kumshitaki Afisa mkuu Sam Rush wakimtaka alipe £7m, kwa madai yanayohusiana na gharama za uhamisho na malipo ya mchezaji wakati wa uongozi wake katika kilabu. (Mail)
 
Ujerumani walishindwa kwa mara ya kwanza katika mechi 23 baada ya mshambuliaji wa Manchester City Gabriel Jesus kuwafungia Brazil bao moja na kuwapa ushindi wa 1-0 jijini Berlin.
Hiyo ilikuwa mara ya kwanza kwa mataifa hayo mawili kukutana uwanjani tangu Ujerumani walipowaaibisha Brazil 7-1 katika nusufainali ya Kombe la Dunia mwaka 2014 mjini Belo Horizonte.
 
Jesus aliwaweka Brazilmbele kwa mpira wa kichwa dakika za mwishi mwisho kipindi cha kwanza, dakika ya 37.
Alikuwa amepoteza nafasi nyingine ya kufunga muda mfupi awali na kipindi cha pili alipoteza nafasi nyingine pia ambapo aliumpiga mpira nje kwa kichwa lango likiwa wazi baada ya Trapp kutokea kujaribu kuudaka mpira kona ilipopigwa
 
Mjerumani Julian Draxler apia alipoteza nafasi ya kufunga mechi ikikaribia kumalizika.
Hii ilikuwa mara ya kwanza kwa Ujerumani ambao ni mabingwa watetezi wa Kombe la Dunia na walioorodheshwa nambari moja duniani kushindwa tangu walipolazwa na Ufaransa nusufainali Euro 2016.
 
Tangu wakati huo, vijana hao wa Joachim Low walikuwa wameshinda mechi 16 na kutoka sare mechi sita kabla ya mechi hiyo iliyochezewa uwanja wa Olympiastadion.
Brazil kulipiza kiasi
Ingawa ilikuwa mechi ya kirafiki, ushindi huo ni wa maana sana kwa Brazil ambao wameandamwa na kushindwa kwao Kombe la Dunia miaka minne iliyopita nchini mwao.
 
Kabla ya mechi, mkufunzi wao Tite aliyepewa kazi mwaka 2016 alikuwa amesema: "Hii ina maana kubwa sana kisaikolojia - hakuna anayehitaji kujidanganya kuhusu hilo," Titea aliambia jarida la Kicker.
"Matokeo hayo ya 7-1 ni kama mizimu, watu bado huyazungumzia. Kadiri unavyoyazungumzia zaidi, ndivyo mizimu hii inavyochukua muda mrefu kutoweka."
 
Nilikuwa ninatazama mechi hiyo (ya mwaka 2014) niliwa nyumbani Sao Paulo na mke wangu na baada ya bao la tatu kufungwa, alianza kulia," amesema Tite.
"Hili lilinigusa sana, nami nikaanza. Ulikuwa wakati mzuri sana kwa Ujerumani, kila kombora lililolenga goli lilikuwa bao - mambo kama hayo huwa hayatokei hata kwenye michezo ya video ya kompyuta."
 
Back
Top Bottom