Anza zoezi hili kwa mambo madogo madogo kama kula chakula. Unajua siku hizi watu hata hawafurahii tena hata ladha za vyakula kwa sababu akili zao hazipo kwenye chakula wanachokula. Mtu anakula huku yupo kwenye mitandao ya kijamii, hivyo zoezi zima la kula linakuwa kama kitu cha kupita tu. Hivyo anza kuweka uwepo wako kiakili kwenye zoezi kama la kula, na fikiria kile chakula unachokula, tafuna vizuri, sikia kila ladha ya kilichopo kwenye chakula.