Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Ibrahimovic ndiye mfungaji bora wa muda wote wa Sweden akiwa na mabao 62, katika mechi 116, mara mbili amekuwa mfungaji bora wa Serie A na mara tatu Ligue 1.



Sasa Zlatan anataka kuendeleza onyesho lake kwa kutwaa taji la MLS.
 
JOSE Mourinho ameshaweka wazi usajili wa aina gani atahitaji kufanya katika dirisha lijalo la uhamisho wa wachezaji katika majira ya kiangazi.

Mourinho, anataka kuleta kiungo mpya wa kati kwenye kikosi chake cha Manchester United, ili kuchukua mikoba ya Michael Carrick, ambaye atastaafu mwishoni mwa msimu huu.
 
Kuna orodha ya mastaa kibao imeshawekwa hadharani na Mourinho kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana na kuna majina sita ya viungo wa maana kabisa ambao wanaaminika kuwa na viwango vinavyokidhi kwenda kuichezea Man United. Lakini, ni nani hasa atakayefiti kwenda kucheza sambamba na Nemanja Matic kwenye kiungo ya wababe hao wa Old Trafford?
 
Arturo Vidal (Bayern Munich)

Vidal atakuwa na umri wa miaka 31 wakati msimu ujao utakapoanza na anatarajia kuachana na Bayern Munich kwenye dirisha lijalo baada ya Leon Goretzka kutua kwenye timu hiyo akitokea Schalke. Licha ya kuwa na umri mkubwa, Vidal bado kiwango chake kipo juu akiwa kiungo matata kabisa uwanjani akisaidia kwenye kuzuia na kushambulia. Mourinho imekuwa tabia yake ya kusajili wachezaji wenye uzoefu, hivyo itakuwa si kitu cha ajabu kama Mreno huyo atahitaji kufanya kazi na kiungo huyo huko Old Trafford. Hakuna shaka Vidal atakwenda kufiti kwenye mfumo wa Man United, shida moja tu kama Mourinho atakubali kumpa uhuru uwanjani hasa kutokana na kocha huyo kusema kwamba hatoi tu uhuru wa burebure kwa mchezaji.
 
Marco Verratti (PSG)

Kama Mourinho atahitaji kusajili mchezaji ambaye ataifungua ngome ya mabeki wa timu pinzani, basi Marco Verratti ni mtu sahihi. Kiungo huyo Mtaliano umri wake ndiyo kwanza miaka 25 na anatajwa kuwa mmoja wa viungo wenye ubunifu mkubwa katika katika soka jambo litakalomfanya aje kuwa matata kama atacheza pembeni ya Matic katika kiungo hiyo ya Man United. Uwezekano wa Verratti kuondoka kwenye kikosi cha Paris Saint-Germain kwenye dirisha lijalo ni mkubwa na Mourinho atakuwa amefanya kitu kizuri kama atafanikiwa kunasa huduma ya supastaa huyo wa kimataifa wa Italia. Verratti ataweza kumfanya Paul Pogba kuwa na uhuru ndani ya uwanja baada ya kocha Mourinho kuripotiwa kwamba ameamua kubaki na kiungo huyo kwenye kikosi chake kwa msimu ujao.
 
Sergej Milinkovic-

Savic (Lazio)

Kumnunua Milinkovic-Savic itakuwa kitu cha bahati nasibu kwa Mourinho kwa sababu kuna uhakika mkubwa atakuwa hajamaliza tatizo linaloikabili timu yake na atakuwa amesajili wa wachezaji wa aina ileile. Kiungo huyo wa Lazio, umri wake ni miaka 23 na kwa msimu huu amekuwa akicheza kwa kiwango kikubwa sana na ndiyo maana klabu nyingine zinahitaji huduma yake. Lakini, ukweli ni kwamba Mourinho anahitaji kiungo ambaye atakuwa na majukumu ya kusaidia kwenye safu ya ulinzi, hivyo itakuwa ujinga mkubwa kama ataamini kuwa Milinkovic-Savic ana uwezo wa kwenda kukidhi matakwa yake. Kiungo huyo amefunga mabao tisa na kwa sasa ni jambo gumu kugomea kwamba hatacheza kwenye kikosi cha Man United, lakini usajili wa mchezaji huyo huko Man United ufanyike tu kwa kuwa ni mchezaji kijana kwa matumizi ya siku za baadaye
 
Jean Seri (Nice)

Seri yupo kwenye rada za klabu kubwa nyingi sana za Ulaya kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita kutokana na kiwango chake bora anachokionyesha huko Nice. Ni kiungo mwenye kipaji kikubwa. Kwenye kikosi cha Nice, Seri amepewa majukumu ya kushambulia na kitu kibaya ni kwamba ametoa asisti nne tu. Kama ilivyo kwa Milinkovic-Savic na Verratte, Seri si mchezaji wa kumtegemea sana kwenye kukaba licha ya huko Nice wamekuwa wakimwiita kuwa ni ‘N’Golo Kante wa Nice’. Seri ni kiungo anayependa zaidi kuwa mbunifu wa kutengeneza nafasi ndani ya uwanja kuliko kukaba, hivyo kwa mtindo wa Mourinho litaweza kuwa tatizo halijamalizwa
 
Jorginho (Napoli)

Sehemu bora kabisa ya kikosi cha Napoli. Jorginho mara nyingi amekuwa akicheza kiungo ya chini na kupanga mipango yake hapo huku Allan akiwa na majukumu ya kukaba. Kutokana na hilo, Mourinho akifanikiwa kumnasa Jorginho, basi ataweza kuja kuwa pacha wa Matic, ambaye mmoja atakuwa anakaba tu na mwingine anasambaza mipira kwa wachezaji wa eneo la ushambuliaji kama Alexis Sanchez na Paul Pogba au Juan Mata kuwalisha washambuliaji wa kati. Kimsingi kama kuna kiungo ambaye Mourinho atapaswa kuweka mkazo katika kuipata huduma yake katika dirisha lijalo la usajili kwa sababu ndiye mchezaji anayetazamwa atakuja kuifanya kiungo ya wababe hao wa Old Trafford kukaa sawa.
 
Fred (Shakhtar

Donetsk)

Staa huyo anawindwa pia na Manchester City akitakiwa kwenye dirisha lijalo la usajili. Jambo hilo linafanya kuwapo na uhakika kwamba Fred atatua kwenye soka la England msimu ujao. Man United wanamhitaji kiungo huyo na kocha Mourinho anaamini atakuwa mtu mwafaka kuchukua nafasi ya Carrick na kucheza sambamba na Matic. Fred akija kwenye kikosi hicho cha Old Trafford jambo hilo litampunguzia majukumu Matic na atakuwa na kazi moja tu ya kuwalinda mabeki wa kati na staa huyo wa Shakhtar atakuwa anachukua mipira na kutawanya tu uwanjani kwenda pande zote za uwanja kwa pasi ndefu na fupi.
 
Toni Kroos

(Real Madrid)

Hakuna asiyefahamu soka la kiungo wa Kijerumani, Toni Kroos na anachokifanya huko Real Madrid. Kiungo huyo anacheza soka maridadi na Mourinho atakuwa amefanya bonge la usajili kama atafanikiwa kuinasa huduma ya kiungo huyo anayefanya mambo yake chini ya kocha Zinedine Zidane huko Santiago Bernabeu. Ripoti zinadai kwamba Kroos anaweza kufungua milango ya kutokea Bernabeu kwenye dirisha lijalo baada ya mabosi wake kuonekana kufanya uwezekano mkubwa na pia staa huyo mwenyewe akitaka kwenda kukumbana na changamoto tofauti za usajili.
 
Screenshot_2018-03-29-22-53-52.jpg
 
Back
Top Bottom