Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Ni hapo kwenye usajili ndipo panapopatikana hayo mambo ambayo ni vigumu kuzuilika. Kuna wachezaji itakuwa kasheshe kubwa kuwazuia wasiondoke wakati dirisha hilo litakapofunguliwa na itakuwa bahati kwa timu zao kama wataendelea kubaki hadi wakati dirisha la usajili wa wachezaji litakapofungwa. Kuwabakiza hawa itakuwa kasheshe kubwa.
 
1.Mohamed Salah

(Liverpool)

Fainali za Kombe la Dunia 2018 zitakwenda kufungua soko zaidi la Mohamed Salah na kuifanya Liverpool kuwa kwenye presha kubwa juu ya hatima ya mchezaji huyo. Kuna uwezekano mkubwa akawaacha wakati dirisha la usajili litakapofunguliwa.
 
Real Madrid inatajwa kumhitaji na Barcelona pia inaweza kuingia vitani kwenye mpango wa kuinasa huduma ya supastaa huyo wa kimataifa wa Misri huku matajiri wa Ufaransa, Paris Saint-Germain, nao wakiwa kwenye foleni ya kupigania huduma yake itakapoonekana inaweza kumng’oa kutoka Anfield.
 
2.Antoine Griezmann

(Atletico)

Staa mwenye ofa kibao mezani. Timu nyingi zinahitaji kuwa na Griezmann kwenye vikosi vyao na jambo hilo linaweka ishara kubwa kwamba staa huyo wa kimataifa wa Ufaransa hawezi kuendelea kubaki Atletico Madrid baada ya msimu huu kumalizika.
 
Barcelona ndiyo inayopewa nafasi kubwa ya kuinasa huduma yake licha ya kuwapo na timu nyingine zinazomhitaji pia kama vile Manchester United na vigogo wengine wa Ligi Kuu England.
 
Mkataba wa Griezmann katika kikosi cha Atletico utafika tamati mwaka 2022, lakini hilo haliwezi kuwa kikwazo cha kumfanya asiachane na timu hiyo kutokana na ukweli kwamba hata mwenyewe anahitaji jambo hilo litokee kwenye dirisha lijalo.
 
3.Dele Alli

(Tottenham)

Staa wa Tottenham, Dele Alli, kwa muda mrefu amekuwa akihusishwa na mpango wa kuhamia ng’ambo huku Real Madrid ikitajwa inaweza kuwa sehemu mwafaka atakayokwenda kuibukia. Kwenye fainali zijazo za Kombe la Dunia, Dele ni miongoni mwa wachezaji watakaompasua kichwa Kocha Gareth Southgate katika uteuzi wa kikosi cha kwanza cha England atakachotaka kuanza nacho.
 
Kiwango cha Dele kwa sasa kimeshuka, lakini hilo halina maana linaweza kumtibulia nafasi yake ya kupata timu ya kwenda kuichezea kwa msimu ujao ambao dalili ni kubwa kwamba huenda asiendelee kubaki kwenye kikosi hicho kinachoshiriki mikikimikiki ya Ligi Kuu England.
 
4.Xherdan Shaqiri (Stoke)

Kuhusu CV tu, Shaqiri mambo yake yanatisha. Lakini, kitu kimoja kilichobaki kwa supastaa huyo wa kimataifa wa Uswisi ni kukihamisha kikosi chake kutoka kwenye ubora na kuwa bora zaidi. Ana medali ya ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya aliyobeba akiwa na Bayern Munich. Shaqiri bado kuna kitu hajakifanya kitakachomfanya kuthibitisha uspesho wake. Amekuwa akionyesha ubora wake wa kufunga mabao ya aina tofauti na huduma yake kwa sasa anaitoa huko kwenye kikosi cha Stoke City.
 
Umri wake ni miaka 26 na msimu huu amefunga mabao 13 ya Ligi Kuu England katika kikosi chake cha Stoke, rekodi ambayo si mbaya kwa vile timu hiyo kwa jumla imefunga mabao 29 tu. Ukweli ni kwamba Shaqiri si mchezaji wa kuichezea Stoke na ndio maana haionekani kama ataendelea kubaki kwenye timu hiyo baada ya msimu huu kumalizika.
 
5.Alexsandr Golovin (CSKA)

Kihistoria, timu inayokuwa mwenyeji wa Kombe la Dunia mara nyingi imekuwa ikiibuka na mastaa kadhaa wakali ambao fainali hizo zinapofika mwisho tu, basi na wachezaji hao wanapata dili la kujiunga na timu nyingine tofauti na zile walizokuwa wakichezea.
 
Kwenye kikosi cha Russia msimu huu, kuna staa anaitwa Alexsandr Golovin, ambaye kimsingi anatazamwa atakwenda kufanya mambo ya maana ambayo hakika yatamfanya awe na dili kibao kwenye meza yake zinazohusu usajili. Timu anayochezea Golovin kwa sasa ni CSKA Moscow. Umri wake ni miaka 21 tu na kiungo huyo ana kipaji kikubwa kinachomfanya kuwindwa na timu za maana kama Barcelona na Arsenal.
 
Back
Top Bottom