Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

3. Upungufu Wa Potashi (Potassium)
Kupungua kasi ya ukuaji wa mimea, ambayo inasababisha mmea kudumaa.
Upungufu ukiwa mkubwa rangi ya kijani inafifia na mwisho kutoweka kabisa na sehemu iliyoathirika inakauka (necrosis) kwenye mazao mengi , mazao mengine ya nafaka na miti ya matunda. Kutoweka kwa rangi ya kijani na kukauka kunaanzia pembeni mwa majani na kwenye ncha. Majani yanakuwa na michirizi ya manjano na vinundu nundu kama migongo ya bati (yellowish streaks and corrugated). Majani ya mwanzo hukauka mapema kwenye mimea yenye upungufu kuliko ile yenye potashi ya kutosha.
 
JINSI YA KUTUMIA MBOLEA WAKATI WA KUPANDA Wakati wa kupanda, mbolea kama vile Yara Miller Winner, au NPK, DAP, MiNJINGU AU TSP, zitakufaa, ila ni bora zaidi kama utatumia DAP kipimo kama gram10 sawa na kifuniko kimoja cha maji ya uhai mfuko 1 unatosha kwa hekari moja angalizo mbolea a viwandani zisichanganyike na mbegu. kama utatumia samadi ni vizuri zaidi kiasi cha mkokoteni 1 kitatosha kwa hekari moja ila kama utatumia samadi hakikisha ukisha iweka kwenye masimo acha kwa muda wa wiki moja alafu panda
 
JINSI YA KUTUMIA MBOLEA WAKATI WA KUKUZIA KARANGA(KARANGA HAZIITAJI SANA MBOLEA)
Utahitaji mbolea kama vile, CAN, UREA, AU NPK, Au Yara Miller winner, changua moja kati ya hizo kipimo ni Gram 10 sawa na kifuniko cha soda au maji safi kwa kila mmea kwa hekari moja utatumia kama mfuko mmoja
 
Red Mwitunde
Ilitolewa kwa wakulima miaka ya 1950.
Mbegu za muda mrefu (Virginia Spreading bunches).
Huchukua muda wa siku 120 -140 toka kupanda hadi kukomaa. Ina uwezo wa kutoa kilo 1000 kwa hekta. Mbegu zake ni kubwa na zina rangi nyekundu.
 
b. Nyota
Ilitolewa mwaka 1983.
Mbegu ya muda mfupi( Spanish Errect Banch).
Huchukua siku 90-100 tangu kupanda hadi kukomaa. Ina uwezo wa kuzaa wastani wa kilo 1500 kwa hekta. Mbegu zake ni ndogo, na zina rangi ya udongo (Tan).
Aina hii ya mbegu zina tabia ya kuanza kuota tena shambani mara tu zikiisha komaa, hivyo ni muhimu kuzivuna mapema zikisha komaa.
 
c. Johari:
Ilitolewa mwaka 1985.
Mbegu ya muda wa kati (Virginia Spreading Bunches).
Huchukua siku 110 - 120 toka kupanga kuvuna. Mbegu zake ni kubwa na zina rangi ya udongo (Tan). Ina uwezo wa kutoa wastani wa kilo 1000 kwa hekta moja.
 
d. Pendo: .
Ilitolewa mwaka 1998.
Mbegu ya muda mfupi ( Spanish Errect Banch). Huchukua siku 90-100 tangu kupanda hadi kukomaa. Ina uwezo wa kuzaa wastani wa kilo 1500 kwa hekta. Maganda yake ni laini na mbegu zake ni kubwa, na zina rangi ya udongo (Tan). Kama Nyota, aina hii ya mbegu ina tabia ya kuanza kuota tena shambani mara tu zikisha komaa, hivyo ni muhimu kuzivuna mapema zikisha komaa.
 
e. Sawia:
Ilitolewa mwaka 1998.
Mbegu ya muda wa kati (Virginia Spreading Bunches).
Huchukua siku 110 - 120 toka kupanga kuvuna. Mbegu zake ni kubwa na zina rangi ya udongo (Tan). Ina uwezo wa kutoa wastani wa kilo 1000 kwa hekta moja.
Pamoja na mbegu zilizotajwa, kuna aina nyingine nyingi za kienyeji (local varieties) zinazotumiwa na wakulima katika sehemu mbali mbali.
 
UTAYARISHAJI WA SHAMBA
Shamba litayarishwe vizuri kuwezesha udongo kupenyesha maji na mizizi kirahisi. Karanga hupandwa kwenye matuta au sensa (shamba tambarare).
 
UTAYARISHAJI WA MBEGU
Karanga ambazo zinakusudiwa kwa mbegu zitunzwe na maganda yake bila kubanguliwa. Zibanguliwe karibu na msimu wa kupanda na kuchaguliwa. Baada ya kuchaguliwa zitiwe dawa, aina ya Fernasan D, Katika uwiano wa gramu 28 za dawa kwa kila kilo 10 za mbegu safi.
 
WAKATI WA UPANDAJI
Uamuzi wa kuchagua wakati mzuri wa kupanda niule utakaoliwezesha zao hilo kukomaa wakati wa mvua za mwisho. Kuchelewa kupanda, hupunguza mavuno. Ni muhimu kuchagua aina ya mbegu ambazo uvunaji wake unafanana na mazingira ya eneo hilo kihali ya hewa.
Kwa mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma, karanga za muda wa kati na mrefu (Johari, Red Mwitunde) zipandwe kuanzia katikati, hadi mwishoni mwa mwezi Desemba. Karanga za muda mfupi (Spanish na Valencia) zipandwe kuanzia mwishoni mwa mwezi Desemba hadi katikati ya mwezi Januari.
Kwa mikoa ya Tanga, Morogoro na sehemu za mkoa wa Dodoma, karanga zipandwe mapema mwanzo wa mvua ndefu. (Februari/March).
 
NAFASI KATI YA MIMEA
Inashauriwa kupanda karanga katika mistari. Nafasi kati ya mistari ni sentimita 50, na kati ya mimea ni sentimita 15, kwa karanga zinazotambaa (Virginia Spreading types). Kama karanga zinapandwa kwenye matuta ya sentimita 90, zipandwe mistari miwili, kila tuta. Kwa nafasi hii kiasi cha kil 60-75 za mbegu hutumika kwa hekta moja.
 
Kwa karanga zilizopo kwenye kundi la Spanish/Valencia (zisizotambaa), nafasi kati ya mistari ni sentimita 50, na kati ya mimea ni sentimita 10. Endapo karanga zimepandwa kwenye matuta ya sentimita 90, panda mistari miwili , inayofanya nafasi sawa na sentimita 50 kwa sentimita 10. Kiasi cha kilo 80-100 za mbegu hutumika kwa hekta moja kwa kutumia nafasi hii.Kwa ina zote za mbegu, panda mbegu moja safi, katika kila shimo.
 
Karanga NACHI 2015
·Inastawi katika ukanda wa chini na katikatika mwinuko wa mita 0 hadi 1,500.
·Inakomaa kwa siku 110.
·Inastahimili ugonjwa wa ukoma wakaranga (groundnut rosette).
·Inatoa mavuno ya wastani wa tani 1.1hadi 2 kwa hekta.
· Mbegu zake ni kubwa na zinafaa kwaajili ya wasindikaji wa karanga zakutafuna ( confectionary market).
 
KUCHELE2015
·Inastawi katika ukanda wa chini na katikatika mwinuko wa mita 0 hadi 1,500.
·Inakomaa kwa wastani wa siku 102 hadi110.
·Inastahimili ugonjwa wa ukoma wakaranga (groundnut rosette)
·Inatoa mavuno ya wastani wa tani 1.2kwa hekta.
·Majani yake yamejikunja kwa ndani naMbegu zake zina rangi ya kahawia
 
NARINUT2015
·Inastawi katika ukanda wa chini na kati
katika mwinuko wa mita 0 hadi 1,500.
·Inakomaa kwa wastani wa siku 106 hadi110.
·Inastahimili ugonjwa wa ukoma wakaranga (groundnut rosette).
·Inatoa mavuno ya wastani wa tani 1.3hadi 2 kwa hekta.
·Mbegu zake ni kubwa na zinafaa kwaajili ya wasindikaji wa karanga zakutafuna ( confectionery market).
·Mbegu zake zina rangi ya kahawia.
 
MBOLEA
Kufuatana na majaribio yaliyofanyika imeonekana kuwa karanga hustawi vizuri chini ya viwango vidogo vya phosphorus (TSP, SSP). Vile vile katika sehemu nyingine, karanga zimefanya vizuri kwa kutumia samadi. Ubadilishaji wa mazao (Crop Rotation) husaidia kutunza rutuba, hivyo kupunguza kiasi cha mbolea kinachotumika.Karanga zinaweza kulimwa baada ya mahindi, ili kutumia masalia ya mbolea.
 
UPALILIAJI
Karanga zipaliliwe zikiwa changa. Shamba lililotayarishwa vizuri na kuondolewa magugu ya muda mrefu (Perrenial weeds) linaweza kupalliwa mara moja, kwa sababu karanga hukua haraka, na zinaweza kushindana na magugu. Baada ya kutoa maua, karanga zisipaliliwe, hii inaweza kuharibu 'pegs', hatimaye kupunguza mavuno.
 
MAGONJWA NA WADUDU WAHARIBIFU:
1. MAGONJWA
(i) Ugonjwa wa kuoza (Aflatoxin)
Katika hali ya unyevu mwingi vimelea viitwavyo Aspegilus flavus huota ndani ya maganda na kushambulia mbegu za karanga. Vimelea hivyo hutoa kemikali ambayo ni sumu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…