Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Ndinga
IMG-20180328-WA0013.jpg
 
MWANAMUZIKI Kanye West ameachana rasmi na meneja wake, Izvor Izzy ikiwa ni miaka minane baada ya kufanya kazi pamoja.

Mtandao wa TMZ umeandika kuwa wawili hao kwa sasa hawako pamoja na wamevunja kabisa mkataba wao.
 
Imedaiwa jukumu la usimamizi wa kazi za Kanye kwa sasa limechukuliwa na meneja wa Justin Bieber, Scooter Braun.

Si Kanye wala Izvor ambaye alikuwa tayari kuweka wazi sababu za kutengana kwao ingawa inadaiwa kuna Izvor alishindwa kutekeleza majukumu yake jambo lililosababisha moja wapo ya dili la Kanye liharibike.
 
MSANII anayekuja juu katika muziki wa kizazi kipya anayefanana kimwonekano na Mmarekani, Lil Wayne, Said Rashid ‘T- Wayne’ ameanza mambo kwa kuachia ngoma mpya iitwayo ‘Am So Lost’.

Wimbo huo ameurekodia nchini Msumbiji na T Wayne ametamba kuwa hizo ni salamu zake kwa wana hiphop wengine nchini kutaka kuthibitisha kuwa hajaingia kwenye gemu kimakosa, bali ni kipaji alichozaliwa nacho.
 
Nataka kutofautisha kazi zangu na za wanahiphop wengine, mashabiki wasidhani nimejitosa huku kwa sababu ya kufanana na Lil Wayne, bali nina kipaji na kupitia ngoma hii salamu zangu zitafika kabla ya kuanza ziara ya kuitambulisha,” alisema.
 
Mwimbaji huyo alisema. baada ya kuutambulisha jijini Dar es Salaama ataanza kazi ya kurekodi video kisha kuanza mipango ya kuachia kazini nyingine mpya, huku akisisitiza umefika wa kuwepo kwa mabadiliko katika miondoko ya hip hop.
 
Akiwa katika mahojiano ya pamoja na Selma Blair na Christina Aguirela, Diaz alisema muda si mrefu ataungana na wenzie hao kupumzika kwa hakuna analolifanya kwa sasa kwenye fani.

“Sina ninachokifanya naweza kusema nipo kama sipo huenda wakati umefika wa kugeukia upande mwingine.”
 
Wakati waumini wa dini ya Kikristo nchini wakiungana na wenzao duniani kote kusherehekea Sikukuu ya Pasaka, wachambuzi wa masuala ya siasa, uchumi na jamii wanatarajia kusikia ujumbe kuhusu amani, upendo na mshikamano.

Kadhalika, baadhi yao wamesema wanatarajia viongozi wa dini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) na Baraza la Maaskofu Katoliki (TEC) kutoa ufafanuzi zaidi wa waraka waliotoa hivi karibuni kuhusu masuala ya kijamii, kiuchumi, kisiasa na kimaendeleo.
 
Akizungumza na Mwananchi, wakili wa kujitegemea kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, Harold Sungusia alisema hivi karibuni viongozi wa KKKT na TEC, walitoa matamko yaliyozungumzia hali halisi ya nchi katika masuala ya demokrasia na maendeleo.

Alisema baada ya matamko hayo kumekuwa na mijadala mingi ya kupinga na kuunga mkono, hivyo watumie sikukuu hiyo kufafanua matamko hayo kama kuna jambo jipya wamelisikia baada ya kuyatoa.
 
Februari 10, Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) lilitoa ujumbe wa Kwaresma wa mwaka 2018 ndani yake likitoa msimamo kuhusu masuala ya kisiasa, kiuchumi na kijamii.

Ujumbe huo ulioandikwa na maaskofu wote 35 wa TEC wakiongozwa na rais wao, Mhashamu Tarcisius Ngalalekumtwa ulizungumzia hali ya kisiasa nchini kwa kuonya uamuzi wa Serikali kuzuia maandamano na mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa ni kwenda kinyume cha Katiba ya nchi.
 
Back
Top Bottom