Wakati waumini wa dini ya Kikristo nchini wakiungana na wenzao duniani kote kusherehekea Sikukuu ya Pasaka, wachambuzi wa masuala ya siasa, uchumi na jamii wanatarajia kusikia ujumbe kuhusu amani, upendo na mshikamano.
Kadhalika, baadhi yao wamesema wanatarajia viongozi wa dini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) na Baraza la Maaskofu Katoliki (TEC) kutoa ufafanuzi zaidi wa waraka waliotoa hivi karibuni kuhusu masuala ya kijamii, kiuchumi, kisiasa na kimaendeleo.