Ronaldo amefunga mabao 19 mechi zake tisa za karibuni zaidi akichezea Real - 25 mechi 13 alizochezea nchi yake na klabu karibuni zaidi
Amefunga mabao 39 mechi 36 alizochezea Real msimu huu - mabao mengi kushinda mchezaji mwingine yeyote yule anayecheza ligi tano kuu za Ulaya (England, Ufaransa, Ujerumani, Italia na Uhispania)
Amefunga mabao katika mechi 10 alizocheza karibuni zaidi Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya mtawalia - tisa msimu huu na wakati wa fainali msimu uliopita - kwa jumla amefunga mabao 16
Ronaldo ndiye mfungaji mabao bora Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya akiwa na mabao 119 - mabao 19 mbele ya Lionel Messi wa Barcelona.
Amefunga mabao tisa kati ya makombora yake 11 yaliyolenga lango dhidi ya kipa maarufu Gianluigi Buffon.
Ronaldo amekuwa akifungia Real Madrid bao la kwanza mechi za Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya katika mechi 10 kati ya 14 walizocheza karibuni zaidi
Amefunga mabao 22 robofainali Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya, moja zaidi ya Juventus. Ni timu tano pekee, ikiwemo Real Madrid, ambazo zimefunga zaidi ya hapo hatua hiyo.
Ronaldo amefunga (14) au kusaidia ufungaji (mara tatu) 68% wa mabao yote 25 ya Real Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya msimu huu
Amefunga katika kila mechi sita alizocheza dhidi ya Juventus - mabao tisa kwa jumla. Hakuna mchezaji aliyefunga mabao zaidi dhidi ya timu moja Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kuliko yeye.