Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Shoo ya mwanamuziki wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Werrason Ngiama iliyokuwa ifanyike leo Ijumaa Aprili 6, 2018 kwenye ukumbi wa Escape One imeahirishwa kutokana na mwanamuziki huyo kuchelewa kufika nchini.

Kuchelewa huko kumetokana na hati za kusafiria za Werrason na wanamuziki wake nchini DRC kuchelewa, hivyo kukwamisha taratibu nyingine za kusafiri.
 
Taarifa za kuahirishwa kwa shoo hiyo zimetolewa leo na Katibu Mkuu wa Chama cha Muziki wa Dansi Tanzania (Chamudata), Hassan Msumari.

“Kundi hili litaingia nchini Tanzania kesho Jumamosi na wote waliokata tiketi za onyesho la Escape One wazitunze kwa ajili ya kuzitumia tarehe itakayotangazwa la kundi zima la Wenge Mason Mere linaingia Jumamosi,” amesema Msumari.
 
He!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…