Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Keep Moving
GBWA-20180225064818.jpg
 
Siku zote katika maisha njisi unavyoonekana ni matokeo ya lishe yako ya kila siku.Tangu unapokula asubuhi mpaka jioni huamua afya ya mwili wako iweje.Hivyo basi hata katika swala zima la afya ya ngozi yako inategemea unakula nini.Kumbuka chakula unachokula kinaweza kikajenga afya yako na kuwa imara au kudhorota afya yako na kuwa dhaifu.
 
Afya ya ngozi yako ni sehemu moja muhimu sana kuipa umakini.Watu wengi huwa hawajui siri iliyopo katika vyakula tunavyokula katika kuboresha au kubomoa afya ya ngozi zetu.Baadhi ya watu huwa wanaangaika kutafuta mafuta ya kikemikali kuhakikisha ngozi zao zinakuwa vizuri pasipo kutambua kile wanachokula ndio kitaamua afya ya ngozi yako iwe katika hali gani. Leo nataka nikufumbue macho katika hili ili ufahamu umuhimu wa vyakula tunavyokula
 
Wataalamu wa afya wanasema kila kitu tunachokula ni sehemu ya miili yetu ikiwa ni pamoja na muonekano wa nje(ngozi).Hivyo kadiri utakavyoendelea kula chakula bora ndivyo afya ya ngozi yako itazidi kuimarika zaidi.
 
Matumizi ya chumi yapo kila siku katika vyakula tunavyokula hasa mida ya mchana na jioni hivyo ni muhimu kuzingatia kiwango cha chumvi kinachoitajika.Chumvi yenye madini ya iodine ni hatari kwa afya ya ngozi yako,husababisha chembechembe za nyama yako katika ngozi kuvimba.
 
Sukari huwa inatumiwa na watu wengi kila siku katika vyakula mbalimbali,lakini kiwango cha sukari kikiwa kingi husababisha ngozi kuwa kavu na kufanya mwili kutengeneza makunyazi kwa sababu inaharibu kemikali ya collegen na elastin zinazofanya kazi ya matengenezo ya ngozi.
 
Vyakula hivi vimetokea kupendwa na watu wengi sana hasa maeneo ya mijini, vyakula kama chipsi, nyama za kukaanga n.k .Vyakula hivi huweza sababisha mafuta mengi kujaa mwilini hasa sehemu za ngozi na kusababisha uzibaji wa vijitundu vidogo vidogo vilivyopo katika ngozi yako.
 
katika kahawa huwa kuna kemikali ya caffeine ambayo usababisha ukosefu wa maji ya kutosha katika ngozi yako na kuifanya kuwa kavu wakati wote.Pia kemikali hii ya caffeine husaidia kutengeneza kimekali ya cortisol inayosababisha ngozi kuzeeka mapema.
 
Swali:Je kuna vyakula vinavyoweza kuboresha afya ya ngozi yangu?

Jibu ni ndio ,kama nilivyosema mwanzo ulaji wetu husababisha kuboresha au kudhoofisha afya ya ngozi zetu.Mpaka sasa umeona vyakula vinavyodhoofisha afya ya ngozi yako. Ni vyema ukaanza kula vyakula hivi ambayo vitaboresha afya ya ngozi yako.
 
Vyakula hivi ni muhimu sana kwa afya ya ngozi yako huwa vimesheeni aina mbalimbali za vitamini vyenye faida katika ngozi na mwili wako kwa ujumla .Mboga za majani husaidia katika uzalishaji wa seli mpya katika mwili wako na kuondoa seli zile zilizokufa.Hivo upelekea ngozi kuwa yenye kung'ara na kuvutia pia.
 
Back
Top Bottom