Tunaona ni kwa namna gani tunavyopoteza nguvu kazi ya Taifa kwa maradhi yanayoweza kutibika na kuyakinga kabla hayajawadhuru walengwa. Imeelezwa pia saratani hiyo ya mlango wa kizazi inachukua asilimia 32.8 ya wagonjwa wote wanaougundulika kuugua saratani nchini kila mwaka. Kwa maana nyingine, saratani ya mlango wa kizazi ndiyo inayoongoza kwa kuua kwa mujibu wa takwimu kutoka Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI). Hivyo, tukiwa Watanzania,