Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mashabiki wa Arsenal waamini kupangwa dhidi ya Atletico Madrid katika Europa Ligi itawapa ‘hukumu sahihi’ kwa sababu Arsene Wenger atatimuliwa wakitolewa au atabaki kwa kuwapa ubingwa na kupata tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa msimu ujao.
 
HATIMAYE mambo yamewekwa wazi. Ni Liverpool dhidi ya Roma halafu Bayern Munich na Real Madrid. Hizi ndizo mechi mbili za nusu fainali Ligi ya Mabingwa wa Ulaya kwa ajili ya kupata wababe wawili watakaokumbana katika pambano la fainali Kiev nchini Ukraine Mei mwaka huu.
 
Ratiba ya mechi hizo ilipangwa jana Ijumaa mchana na staa wa zamani wa AC Milan, Chelsea na timu ya taifa ya Ukraine, Andriy Shevchenko katika jiji la Nyon nchini Uswisi na mechi za kwanza zitacheza Aprili 24 wakati ya pili itachezwa Aprili 25 kwa nusu fainali za kwanzana wiki moja baadaye, zitarudiana Mei Mosi, na Mei 2.
 
Kabla ya kupangwa kwa ratiba hiyo kulikuwa na gumzo kubwa mitandaoni baada ya klabu ya Roma kupitia mtandao wake kuanza kuuza tiketi za mechi za pambano lao dhidi ya Liverpool siku moja kabla ya kupangwa kwa ratiba hiyo. Hata hivyo baadaye Roma waliondoa ratiba hiyo lakini sasa mechi zimekuja katika mpangilio ule ule.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…