Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Waajiri wote si sawa, anachokitafuta mwajiri mmoja kinaweza kuwa tofauti na mwajiri mwengine. Sababu inaweza kuwa ni kuwa mazingira ya kazi ya mwajiri mmoja yanatofautiana na mwajiri mwengine, kwahiyo watakapokuwa wanakusaili watakuwa wanaangalia vitu tofauti kutoka kwako.
 
Kila mwajiri anatafuta stadi za mwombaji zitakazoendana na kazi alizonazo katika ofisi yake ili kuboresha ufanisi wa kazi ili kutoa bidhaa au huduma nzuri kwa wakati na ubora unaotarajiwa na mteja. Lakini nje ya stadi kuna vitu ambavyo waajiri wengi wanafanana katika kuviangalia kutoka kwa mwombaji wa ajira.
 
Habari nzuri ni kuwa watafuta ajira wengi wanazo hizo sifa ila tu wanashindwa kuzionyesha wanapopata nafasi ya kuzionyesha. Na habari nzuri Zaidi ni kuwa kwa wale ambao hawana wanaweza kujijengea tabia hizi na zikawapa nafasi nzuri ya kuajiriwa kwa kupata mtu sahihi wa kuwaelimisha
 
Na habari nzuri Zaidi ni kuwa utakapozijua hizi tabia utaweza kuboresha mfumo wako wa uombaji kwa kuelekeza moja kwa moja katika wasifu wako kile anachotafuta mwajiri katika kazi husika. BAdala ya kujaza masifa kibao katika wasifu wako utajua namna ya kuweka zile za muhimu.
 
UWEZO WA KUWASILIANA




Uwezo wa kuwasiliana upo katika pande tatu moja ni uwezo wa kusikiliza, pili ni uwezo kuongea na tatu ni uwezo wa kuandika. Na kama unavyojua lugha yetu ya kiofisi ni kiingereza sasa ukiwa vizuri katika pande hizo tatu utajiweka katika nafasi nzuri katika soko la ajira.
 
2.UWEZO WA KUTUMIA KOMPYUTA




Hapa tuelewane vizuri, kujua kompyuta haimaanishi lazima uwe umesomea kozi yake miaka kadhaa chuo labda kama kazi unayoomba inahusiana moja kwa moja na uweledi wa kompyuta kwa kusomea kozi husika. Ila kama unaomba kazi ambazo hazina uhusiano wa moja kwa moja na masomo ya kompyuta, nataka nikwambie haimaanishi ndo usijue kitu kuhusu kompyuta.
 
Dunia hii ya utandawazi kila kazi kwa namna moja ama nyingine ili kuikamilisha lazima kompyuta itaingia kati sasa kama hujui kuitumia kabisa utakuwa unajipunguzia soko. Mathalani uweze kutuma barua pepe (E-mail), programu ya maandishi (Microsoft word) na program ya namba na maandishi (Microsoft Excel)
 
3.UWEZO WA KUBADILIKA/KUFANYA KAZI ZAIDI YA MOJA



Katika dunia hii ambayo ukuaji wa teknolojia na ushindani wa huduma na bidhaa umekuwa mkubwa ofisi nyingi hupunguza gharama kwa kuajiri watu wachache wenye uwezo wa kufanya kazi Zaidi ya moja ili gharama za kuzalisha ziwe ndogo na wao waweze kushusha bei kupunguza ushindani na kuliteka soko.

Hivyo ukiwa na sifa ya uelewa wa kazi Zaidi ya moja utajiongezea nafasi katika soko la ajira.
 
4.UWEZO WA KUCHANGANYIKA NA WENGINE




Katika mazingira ya ofisi ambayo binadamu Zaidi ya mmoja wanashirikiana kufanikisha lengo moja la ofisi, uwezo wa mfanyakazi mmoja kuchangamana na mwengine bila tatizo ni jambo la muhimu sana.
 
Ofisi inaweza kuruhusu mtofautiane kwa hoja ili kupata kitu kizuri lakini si kugombana sababu wazo la mmoja limepingwa na wengi na kuwanunia, hii italeta utengano na kushusha ufanisi mahali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…