Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

C227A68E-175C-4C21-9183-E635F3E6D611.png
 
Laurie Notaro aliwahi kusema;

“If you really believe in what you're doing, work hard, take nothing personally and if something blocks one route, find another. Never give up”.
 
Kauli hii ikimaanisha;

“Kama unaamini katika kile unachofanya, fanya kwa bidii, usifanye ubinafsi na kama kuna jambo litajitokeza kufunga njia moja, tafuta njia mbadala. Usikate tamaa”.
 
Kukata tamaa ni kitendo cha kuishiwa mbinu mbadala za kukamilisha jambo Fulani ulilokuwa unalifanya kwakuwa tu umekumbana na ugumu. Katika kila jambo tunalofanya huwa tuna matarajio ya kufanikiwa ila pia changamoto haziwezi kuepukika.
 
Maneno “Kata” na “Tamaa” hayatakiwi kuwa pamoja. Hata neno hapana halipaswi kuwa sehemu ya neno katika kamusi yako. Kuwa sehemu ya jamii ya watu Fulani katika dunia unakuwa ni kiumbe wa pekee kuwahi kutembea juu ya ardhi hii.
 
SABABU 8 ZA KWANINI HUTAKIWI KUKATA TAMAA

1.UPO HAI,NA UNAWEZA




Yaani ilimradi una pumua pumzi ya uhai, hakuna uhalali wa wewe kusema kuna jambo limekushinda na unalikatia tamaa. Kama ukiweka akili na mawazo yako katika hilo jambo lazima utaweza kufanya japo kufanikisha sehemu yake. Hakuna lisilowezekana chini ya jua.
 
Christopher Reeve aliwahi kusema;
“So many of our dreams at first seem impossible, then they seem improbable, and then, when we summon the will, they soon become inevitable.
 
Ikimaanisha; “Ndoto zetu nyingi kwa mara ya kwanza huonekana haziwezi kuwa kweli, baadae huonekana haziwezekani kabisa, ila, tunaipoita utayari wa kufanya ndani yetu, punde zinakuwa haziwezi kuepukika”
 
2. AMINI KATIKA NDOTO ZAKO



Ukikata tamaa, unajikatia tamaa mwenyewe na si mtu mwengine yeyote. Usijiuze mwenyewe wala kuruhusu mtu mwengine akurudishe nyuma. Kama unaweza kuwa na ndoto zako mwenyewe basi hata uwezo wa kutimiza unao.
 
2. AMINI KATIKA NDOTO ZAKO



Ukikata tamaa, unajikatia tamaa mwenyewe na si mtu mwengine yeyote. Usijiuze mwenyewe wala kuruhusu mtu mwengine akurudishe nyuma. Kama unaweza kuwa na ndoto zako mwenyewe basi hata uwezo wa kutimiza unao.
 
Chukulia mfano ndugu wawili kutoka katika familia ya Wright waliokuwa wana ndoto za kutengeneza ndege jinsi walivyokumbana na vikwazo vya kuifanya ndogo yao kuwa kweli huku hakuna aliyedhani kama ndoto inawezekana kwa kuwacheka na kejeli. Hawakukatishwa tamaa ila walipambana kuifanya ndoto yao kuwa kweli na walifanikiwa, je usafiri wa ndege si kiunganishi muhimu katika dunia ya leo?
 
Back
Top Bottom