Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Pia Nikki alikanusha ripoti kwamba Rais Trump anampango wa kuviondoa vikosi vya askari wake kutoka Siria ndani ya miezi sita. Nikki pia ameongeza kusema kuwa Washington ilikuwa na nia ya kuhakikisha hakuna matumizi zaidi ya silaha za kemikali huko Syria , na matokeo ya makombora hayo ni kukamilisha kushindwa kwa Kikundi cha Kiislamu cha Kiislamu na kudhoofisha kuenea kwa ushawishi wa Irani katika kanda.
 
Rais wa Marekani Donald Trump ameiambia serikali ya Syria akisema Marekani iko tayari kuishambulia tena ikiwa itafanya shambulizi lingine la kemikali.
Onyo hilo lilikuja bada ya Marekani, Uingereza ba Ufaransa kushambulia vituo vitatu kujibu shambulizi linaloshukiwa kuwa la kememikali kwenye mji wa Douma wiki moja iliyopita.
 
Syria inakana kufanya shaambulizi lolote la kemikali na badala yake inasema kuwa lilifanywa na waasi.
Kura iliyoletwa na Urusi kwa Baraza la usalama la Umoja wa Mataiafa, kulaani mashambulizi yaliyoongoznwa na Matekani ilikataliwa.
Mashambulizi hayo ndiyo makubwa zaidi dhidi ya serikali ya Rais Bashar al-Assad, yaliyofanywa na nchi za magharibi katika kipindi cha miaka saba nchi hiyo imekuwa kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe.
 
Marekani, Uingereza na Ufaransa wamewapa azimio jipya wanachama wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, wakitaka kufanya uchunguzi huru kuhusu matumaini ya silaha za kemikali nchini Syria.
Mipango ya awali ilikuwa imezimwa na Urusi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…