Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

kwa sababu ya mizunguko mingi mara nyingi unaweza kujikuta hutumii maji unatumia soda au juice. Lakini nakushauri tumia maji kila siku asubuhi iwe ndio tabia yako.
 
2.Fanya mazoezi japo dakika 10 mpaka 3o. iwe ni mtindo wako wa kila siku. au kama unaweza kutembea mwendo wa dakika 30 sio mbaya.
 
Kama una gari jaribu kuwa unafanya mazoezi kabla ya kuanza utaratibu wako wa kuondoka. Hii itakusaidia kuondokana na madhara ya kukaa muda mrefu kazini.
 
3.Kula matunda yasio na sukari nyingi au kula mboga za majani kwa kila mlo. Wakati wote fikiria kijani kuwa ndio saladi yako. kipande cha limau, karoti, tango. Sio tu yatakupa lishe bora bali utapunguza uzito mkubwa.
 
4.Ukiwa kazini kila baada ya saa moja simama na ujinyooshe. jaribu kukaa mbali na simu , laptop kwa muda. Ni afya kwa mwili wako na ubongo wako. Sio kazi kubwa ni uamuzi tu.
 
5.Beba karanga ndani ya begi lako , ukisikia njaa kula , inasaidia kukupata nguvu na kuondoa njaa, na kujenga misuli yako vizuri.
 
Tabia bora ya afya ya akili.

1.Panga mawazo yako mwenyewe. Soma vitabu mbalimbali, sikiliza masomo yanayofaa kwenye akili yako. Achana na habari zinazokushambulia akili yako. Uwe na mtazamo ulio wazi, jaribu kusaidia wengine kama unaweza. Pata marafiki wapya, Jifunze njia mpya za mafanikio. Fikiria hekima ambayo unaweza kuijenga ndani ya miaka mitano na zaidi, kama utakuwa mtu wa kuuliza maswali na kutaka kujua
 
2.Waambie kuwa una shukuru kwa kuwa na familia hio, marafiki hao, Waambie maneno mazuri ya upendo, au andika kinote na ukitume , Ni vizuri kuwa mtu wa shukurani kuliko kuwa mtu mwenye woga. Jijenga katika kushukuru kwa kila kitu kilichopo maishani mwako.
 
Maliza siku yako kwa shukurani. Shukuru kwa ajili ya mwenza wako, masomo yako, kazi yako, watoto wako, maisha yako . hii inasaidia kuondoa mawazo mabaya na huzuni yeyote.
 
Screenshot_2018-04-18-13-18-11.jpg
 
3.Jifunze kusikiliza badala ya kujibu. kwa kupata muda zaidi wa kufikiria wakati mtu mwingine anaongea. Hii sio tu inaonyesha kuthamini kile kinachoongelewa , ila inaonyesha kuheshimu na kukubali,pia inakupa muda wa kupima tabia na maneno.
 
Jipe muda wako mwenyewe, maisha yanatokea. utakapokutana na stress, kuchanganyikiwa , hasira, au kutovumilia wakati unapokutana na mambo mengi. Kama utakuwa na muda wako, utaweza kuweka mambo sawa, hutaendeshwa kama robot.
 
Jiambie maneno mazuri kila siku, maneno ya kukutia moyo, maneno ya kukujenga, maneno ya ujasiri, maneno ambayo yatakufanya uwaze mazuri .Jifanyie wema . Unachotaka kufanyiwa wewe, anza kujizoesha kuwafanyia wengine.
 
Back
Top Bottom