Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

KIKOSI cha Chelsea kilicho chini ya kocha Antonio Conte kimetinga hatua ya fainali ya Kombe la Ligi (FA) baada ya kuifunga Southampton mabao 2-0, sasa watavaana na Manchester United.
 
Chelsea imefunga mabao hayo kupitia kwa Olivier Giroud dakika ya 46, baada ya kupokea pasi kutoka kwa Eden Hazard na Alvaro Morata dakika ya 82, akipokea pasi kutoka kwa Cesar Azpilicueta.
 
KWENYE Ligi Kuu England, Arsenal imebakiza mechi tano. Lakini, wana mechi mbili pia za hatua ya nusu fainali kwenye Europa League dhidi ya Atletico Madrid. Ikishinda kwenye nusu fainali hiyo itakayochezwa nyumbani na ugenini, ina maana kikosi hicho kitakuwa na mechi moja zaidi, itakayokuwa ya fainali.
 
Kwa mtazamo huo, kocha Arsene Wenger atakuwa na mechi zisizopungua nane za kucheza kabla hajafungasha virago vyake na kuachana na timu hiyo yenye maskani yake Emirates. Katika mechi hizo zilizobaki, hakuna ukakika kama Wenger atakutana na vipigo vingine vikubwa kama alivyowahi kukutana navyo kwenye maisha yake ya kuinoa Arsenal.
 
Vipigo vizito, ambavyo Wenger alikumbana navyo Arsenal na hawezi kuvisahau ni pamoja na kutupwa nje ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa jumla ya mabao 10-2 kutoka kwa Bayern Munich. Ilikuwa kwenye mechi ya hatua ya 16 bora, ambapo Arsenal ilichapwa 5-1 huko Allianz Arena, kabla ya kuja kurudiwa tena kwa kipigo kama hicho huko Emirates kwenye mechi ya marudiano, miaka miwili iliyopita.
 
Man United 6-1 Arsenal, Februari 2001

Hii ilikuwa mechi ya Ligi Kuu England. Siku hiyo, Dwight Yorke alipiga hat-trick wakati mabao mengine yalifungwa na Roy Keane na Ole Gunnar Solskjaer kuwafanya Manchester United kuongoza 5-1 hadi kufikia mapumzika. Bao la Arsenal lilifungwa na Thierry Henry. Kipindi cha pili, Man United iliongeza bao jingine lililofungwa na Teddy Sheringham na hivyo kumfanya Sir Alex Ferguson kuibuka na ushindi mkubwa dhidi ya mpinzani wake huyo na kuweka pengo la pointi 16 kileleni.
 
Tottenham 5-1 Arsenal, Januari 2008

Hiki ni kipigo kinachouma zaidi kwa Arsenal kupigwa nyingi hivyo na mahasimu wao Tottenham Hotspur. Kipigo hicho si tu kiliwaumiza kuchapwa na wapinzani wao bali kiliwafanya watolewe kwenye michuano ya Kombe la Ligi. Katika mechi hiyo, Spurs ilifunga mabao yake kupitia kwa Jermaine Jenas, Nicklas Bendtner kajifunga, Robbie Keane, Aaron Lennon ma Steed Malbranque kukifanya kikosi hicho cha Spurs kilichokuwa kikinolewa na Juande Ramos kutinga hatua inayofuatia kwa jumla ya mabao 6-2.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…