Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kiongozi wa upinzani nchini Uganda, Dk Kiiza Besigye ameirushia lawama Serikali ya nchi hiyo kwa kuingilia mtandao wake wa kijamii wa Twitter.

Vilevile aliishutumu Serikali hiyo kwa kufuta baadhi ya mambo yake kwenye mtandao wake huo wa kijamii ikiwamo baadhi ya marafiki zake.
 
Akizungumza na gazeti la Daily Monitor kwa njia ya simu, Dk Besigye amesema kwamba ameshangaa zaidi ya marafiki zake 20,000 wakiondolewa kwenye mtandao wake huo ndani ya mwezi mmoja.

Amesema wengi wa marafiki zake hao wanamlalamikia kwamba amewaondoa kwenye orodha ya urafiki.“Nimejaribu kuwatafuta kwenye mtandao, lakini imeonekana kama wamejiondoa kumbe wameshaondolewa muda mrefu na wengi wao wakiwamo marafiki kutoka nchi mbalimbali na humu humu (Uganda),”amesema.
 
Naibu wa Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano serikalini, Kanali Shaban Bantariza amesema Serikali haiwezi kufanya jambo kama hilo.

“Kwa nini Serikali ifute marafiki zake kwenye mtandao huo, kwani inanufaika na kitu gani? Hana cha kusema huyo baada ya kukaa kwa miaka 16 kwenye upinzani, “ amesema.

“Wakati mwingine unipigie kwa mambo muhimu siyo kila kitu Besigye akisema Serikali ijibu.”
 
Wakati watu kadhaa wakihofiwa kufa maji kwa kusombwa na mafuriko kwenye mto Wing'e uliopo mpakani mwa wilaya za Sengerema na Nyang'wale, tayari miili ya watu watano imeopolewa.

Mkuu wa wilaya hiyo, Hamimu Gwiyama amesema kazi ya uokoaji inayofanywa na wananchi wa eneo hilo wamefanikiwa kupata miili hiyo na bado wanaendelea kuwasaka wengine.
 
Gwiyama akizungumza na MCL Digital leo Jumatatu, Aprili 23 amesema maji bado ni mengi na kuwataka wananchi wanaosaka miili kuwa makini kwa kawa hakuna matumaini ya kuwapata hai, hivyo wasihatarishe maisha yao.

Amesema miili minne kati ya mitano iliyoopolewa ni wakazi wa Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza.

"Zoezi linaendelea japo ni gumu kwa kuwa wanatafuta kienyeji hakuna wataalamu wa uokozi ni ‘wananzengo’ wanawatafuta na maji ni mengi kwelikweli," amesema Gwiyama.
 
Mto huo unapokea maji kutoka vijito vilivyopo wilayani Sengerema na Geita na huyapeleka katika Ziwa Victoria na kwamba maji yaliyosababisha maafa hayo yanatokana na mvua iliyonyesha wilayani Geita asubuhi.

Amesema kazi ya kuokoa inaendelea kadri maji yanavyopungua na idadi ya waliokufa inaweza kuongezeka kutokana na watu kulalamika ndugu zao kutoonekana.
 
Wauguzi nchini Zimbabwe wamesitisha mgomo kupinga mazingira mabaya kazini na wameamua kurejea kazini leo Aprili 23.

Makamu wa Rais Constantino Chiwenga wiki iliyopita alitangaza kuwafuta kazi wauguzi 16,000 waliogoma akiwashutumu kutumika kisiasa.

Chama cha wafanyakazi nchini Zimbabwe (ZINA) kimesema jana kuwa mgomo huo umechochewa kisiasa.
 
Ili kutoa nafasi kwa ajili ya kuanzisha upya mazungumzo kuhusiana na madai hayo ya wauguzi ZINA imetoa mwito kwa wauguzi kurejea kazini.

Pia ZINA imefungua shauri mahakamani ikitaka Serikali kubadilisha uamuzi wake wa kuwafuta kazi wauguzi.

Serikali yawafukuza kazi wauguzi wote hospitali za umma
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…