Mara nyingi kutibu jino lililotoboka ambalo halina maumivu ni nafuu Zaidi ukilinganisha na jino lenye maumivu.
Licha ya kung’oa, mgonjwa anaweza kuondokana na tatizo la jino lililotoboka endapo atazingatia ushauri wa daktari. Ushauri ni moja ya matibabu muhimu kwa watu wenye meno yaliyotoboka.
Kwa ushauri wa daktari mgonjwa atapata elimu ambayo wakati mwingine huweza kuwa msaada mkubwa kuliko kung’oa jino husika kama wengi wanavyofikiria. Elimu hii hutolewa kulingana na ukubwa wa athari zilizobainishwa na vipimo.